Wanaomiliki silaha kiholela wapewa siku 30



WAMILIKI wanaomiliki silaha kinyume na sheria wametakiwa kuzisalimisha silaha hizo sehemu husika ndani ya siku 30 zilizotolewa
Amri hiyo imetolewa  jijini Dar es Salaam na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Waziri wa Wizara hiyo Dk. Emmanuel Nchimbi Nchimbi aliviambia vyombo vya habari kuwa hatua hiyo imechukuliwa baada ya kuonekana kuongezeka kwa vitendo vya uharifu ndani ya nchi

Amesema wizara yake imetoa siku 30 kwa wale wote wanaohusika na kumiliki silaha hizo isivyo halali wazisalimishe Jeshi la polisi kituo chochote cha karibu alicho karibu nacho kabla ya msako kuanza Januari mwakani

Amesema wananchi wamekuwa wakifanya matumizi ya silaha kiholela hali inayofanya ongezeko la matukio ya uharifu

Amesema pia watu hao wanaweza kuzisalimisha silaha hizo kwa Watendaji wa Kata, Wenyeviti wa vitongoji, Wakuu wa Mikoa hata wilaya

Amesema endapo muda huo uliotolewa ukimalizika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao ikiwemo na kufikishwa mahakamani kwa kumiliki silaha kinyume cha sheria.



Previous
Next Post »