Mwanafunzi azuiwa kwenda chooni afariki darasani




Katika hali isiyo ya kawaida mwalimu mmoja nchini Misri
anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za mauwaji ya mwanafunzi wa shule ya msingi, baada ya kumfungia darasani na kumzuia kwenda kujisaidia haja ndogo mpaka kupelekea kifo
  

Mwanafunzi mmoja aliyefahamika kwa jina la Ahmed Sultan Abdullah mwenye umri wa miaka 10, amefariki dunia akiwa darasani baada ya kuzuiwa na mwalimu wake kwenda kujisaidia chooni.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea baada ya Ahmed kumuomba mwalimu wake wa darasa amruhusu aende kujisaidiya baada ya kujisikia kubanwa na haja ndogo, lakini mwalimu alikataa ombi hilo na badala yake alimtaka aendele na masomo mpaka hapo kipindi chake kitakapomalizika.

Mwanafunzi alitii amri hiyo na kuendelea na masomo, lakini kila muda ulipokuwa ukienda ndiyo hali ilikuwa ikizidi kuwa mbaya, Ahned aliomba tena ruhusa kwa mwalimu wake, lakini mwalimu alikataa kumruhusu na kuanza kumpiga mpaka kupelekea kifo chake.

Taarifa hiyo imethibitishwa na Meja jenerali mratibu wa maswala ya usalama katika Mkoa wa Assiut, bwana Abu al-Qasim Abu Deif, Abu Deif aliviambiya vyombo vya habari kwamba, mtuhumiwa huyo wa mauaji ameshakamatwa na ameshafiikishwa katika vyombo vya sheria na amefunguliwa mashitaka jalada namba 3924 la mwaka 2012.

Nifahamishe.com ilifika katika eneo la tukio na kubahatia kufanya mazumgomzo na mmoja ya wanafunzi wa shule hiyo ya msingi iliyopo katika mkoa wa Assiut kijiji cha Alvima nchi Misri, mwanafunzi huyo akiongea kwa masikitiko na majonzi makubwa alisema, kwa kweli inasikitisha na inaniuma saana mimi ndiyo mara ya kwanza nashuhudia mtu anakufa alisema mwanafunzi huyo huku akitokwa na machozi.
Previous
Next Post »