'Dola Milioni 5 Kwa Atakayenioa'

NewsImages/6695946.jpg


Mwanamke Mmoja Mfanyabiashara nchini Saudia Arabia ametangaza kutoa donge nono la dola milioni 5 kwa mwanaume yoyote atakayejitokeza na kufunga naye pingu za maisha, ameyasema hayo mbele ya vyombo vya habari 


Mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina moja tu la Masear, amelezea nia yake na kuwataka wanaume wajitokeze kumuoa.

Masear ni mfanyabiashara nchini Saudia na katika maisha yake Masear alibahatika kuolewa hapo awali lakini kwa bahati mbaya aliachika kwa sababu alizozitaja kuwa, mume wake wa kwanza alikua na tamaa ya pesa na alishindwa kutekeleza majukumu yake kama mume.

"Hivi sasa nataka kuolewa sijali ikiwa mume wangu wa sasa atakua na tamaa ya pesa au la, ninachojali mimi nataka kufunga ndoa na mtu anayemudu mapenzi na kutekeleza majukumu yake", alisema Masear.

Masear alitaja baadhi ya masharti ambayo mume wake mpya atalazimika ayatekeleze kuwa ni kuishi katika nyumba yake maalumu iliyopo mkoani Jeddah Saudi Arabia na afuate kila atakachomtaka akifanye.

Masear mwenye umri wa miaka 33, amewataka wanaume watakao kuwa tayari watume maombi yao kwa njia ya Fax au E-mail, watumaji wanatakiwa waambatanishe picha, namba za simu na waweke wazi umri wao.

Vyombo vya habari vya Saudia vimesema kuwa hali kama hii si mara ya kwanza kutokea mwanamke kutangaza hadharani donge nono kwa atakae kubali kufunga naye ndoa.
Previous
Next Post »