Malkia kuhudhuria kikao cha serikali

Malkia Elizabeth

Hapa Uingereza iketangazwa kuwa Malkia Elizabeth atakuwa kiongozi wa kwanza kifalme kuhudhuria kikao cha serikali kwa zaidi ya karne moja iliyopita.

Malkia Elizabeth ambaye amekuwa akijizuia kutoa maoni yake yoyote kisiasa hadharani atakutana na baraza la mawaziri kama sehemu ya kuadhimisha miaka yake sitini ya katika utawala wa kifalme.

Ataondoka kwa kupewa rasmi zawadi na mawaziri kutoka kwenye mifuko yao binafsi kama sehemu ya kuadhimisha miaka yake ya utawala.

Inaaminika kuwa kwa utawala wa kifalme kukaa na baraza la mawaziri mara ya mwisho ilikuwa ni Malkia Victoria, aliyefariki dunia mwaka 1901.
Previous
Next Post »