SERIKALI Mkoani Mbeya imeshauri shule za msingi na sekondari nchini kuwa na utaratibu maalum wa kufundisha watoto suala la kuzingatia usafi wa mazingira hususan kunawa mikono ili kuepukana na magonjwa ya milipuko hususan kipindupindu.


Kauli hiyo imetolewa jana na katibu tawala wa wilaya ya rungwe Moses Mwidete kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas kandoro katika siku ya kunawa mikono duniani iliyofanyika katika viwanja vya jangwani wilayani rungwe mkoani mbeya jana


Alisema kuwa wanafunzi mashuleni wanahitaji kuandaliwa kimtazamo na kifikra ili waweze kuna mfano kwa taifa huko mbeleni ili kupunguza tatizo la mzigo wa kuwaelimisha wanapokuwa watu wazima.


Mwidete alisema kuwa suala la kunawa mikono ni jukuimu la kila mwananchi katika kaya yale husuan kuzungatia kanuni na usafi wa mazingira hususan kwa watoto walio chini ya umri wa mika mitano ambao ndio w aathirika wakubwa kwa magonjwa ya milipuko na kusababisha vifo.

Alisema kuwa hali ya usafi wa mazingira katika nchi yetu si wa kuridhisha hususan katika ujenzi wa vyoo,uthibiti wa taka ngumu,maji taka pamoja na unawaji wa mikopo kwa maji safi na sabuni katika nyakati muhimu ambapo takwimu zinaonyesha %22 ya kaya mijini na %9 vijijini ndizo zina vyoo bora.

"Tafiti zinaonyesha kuwa kunawa mikono kunachangia kupunguza magonjwa ya kuhara kwa kati ya %42 na 50 na kwamba jamii inapaswa kutambua umuhimu wa kujikinga na magonjwa ya milipuko hususan kipindupindu kwa kuzingatia kanuni bora za afya"Alisema.

Aidha aliongeza kuwa vifo vingi vya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano uchangiwa na magonjwa ya kuhara ambapo kila mwaka duniani kupoteza takriban watoto milion 1 na kwa tanzania jumla ya watoto 30,000 ufariki kila mwaka kutokana na ugonjwa wa kuhara.

Kwa Upande wake Afisa Afya Tanzania wizara ya afya na ustawi wa jamii Elias Chinamo alisema kuwa wizara ya afya kushirikiana na wizara ya maji,elimu pamoja na (TAMISEMI) katika baadhi ya halmashauri takwimu zinaonyesha kaya zenye vyoo bora ni asilimia 9.3 ambapo kaya zenye vyombo vya kunawia mikono ni asilimia 3.3 na asilimia 26 hazina vyoo kabisa.

Aidha alifafanua kuwa hii ni changamoto na kwamba bado kuna kazi kubwa inahitajika kufanyika ili kuweza kufikia malengo ya mileniam katika kuongeza upatikanaji wa huduma za usafi wa mazingira katika ngazi ya kaya kwa asilimi 50.
Previous
Next Post »