Akina mama hao wakiwa na hasira kali walisikika wakisema
tuachieni kidogo tumfunze adabu
MWANAMKE
anayetuhumiwa kumtesa kumlisha kinyesi na kumchoma moto mtoto
wa kaka yake kumfungia ndani, amepandishwa kizimbani kwa mara ya pili
katika mahakama ya Wilaya ya Mbeya kujibu
shtaka linalomkabili.
Mwendesha
mashtaka wa Serikali, Achiles Mulisa ameileza Mahakama kuwa
Mtuhumiwa Wilvina Mkandala (24)
Mkazi wa Majengo jijini humo alitenda kosa la kusababisha
majeraha akiwa
na nia ovu ambayo imemsababishia ulemavu mtoto Aneth Gasto
(4).
Mulisa
akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa
mahakama hiyo Gilbert
Ndeuruo amesema kosa hilo ni kinyume cha kanuni ya adhabu
kifungu cha
222(a) sura ya 16 kama ilivyorejewa mwaka 2002.
Kutokana na hali hiyo
mwendasha mashitaka huyo ameileza mahakama kuwa kesi inayo
mkabili mwanamke
huyo ilihitaji mashahidi sita ambao ni Dactari aliye mfanyia
upasuaji mtoto
huyo mwenyekiti wa Mtaa na barozi wake pamoja na
Askari
mpelelezi wa kesi hiyo na mtoto mwenye
.
Amesema
teyari mashahidi wanne kati ya sita wamekwisha toa ushahidi wao
mahakani hapo .
Kutokana
na kosa hilo mshtakiwa amekana shitaka hilo ambapo alirudishwa
mahabusu hadi
Novemba 27 Mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa
tena.
Amesema
upande wa Jamhuri unamashahidi wanne ambao watatu kati yao
teyari wamekwsha toa
ushahidi wao katika mahakama hiyo .
Amewataja
mashahidi hao kuwa ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Majengo Shuku
Mwakanyamale, Daktari
anayemtibu mhanga katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya Dr. Paul
Kasubi na Habiba Mwakanyamale .
Wengine
ni Askari Polisi aliyepeleza kesi hiyo WP Pudensia na Mtoto
mwenyewe ambao wako tayari kufika mahakamani na kutoa
ushahidi wao mbele ya mahakama.
Awali
mshatakiwqa huyo aliieleza mahakama kuwa na uhusiano na mtoto
huyo ambapo
pia alikiri kuwa na taarifa za kile kinachoendelea juu ya
matibabu ya mtoto huyo
na kuhusu kukatwa kwa mkono wake wa kushoto na kufungwa bandeji
ngumu(POP)
kwenye mkono uliobaki.
|
EmoticonEmoticon