Laptop Zinaua Nguvu za Kiume na Kuharibu Mbegu za Kiume



NewsImages/6680522.jpg

Scott Reed alipokuwa akitumia laptop yake mapajani


Imethibitishwa kitaalamu kuwa joto linalotolewa na laptop inapotumika ikiwa mapajani hupelekea kuharibika kwa mbegu za kiume na kuwafanya wanaume washindwe kupata watoto na wapenzi wao


Scott Reed alifikiria kwenda na mkewe hospitali kujaribu njia ya kupandikiza mimba baada ya kuhangaika muda mrefu kujaribu kupata mtoto bila mafanikio.

Kitu ambacho Scott hakuweza kukifikiria ni pale alipoambiwa na madaktari kuwa laptop yake anayoitumia mara kwa mara akiwa ameiweka mapajani ndio chanzo cha tatizo lake la kutopata mtoto.

Madaktari walimuambia kuwa joto linalotokana na laptop yake inapotumika ikiwa mapajani husababisha kuharibika kwa mbegu za kiume na hivyo kumfanya ashindwe kupata mtoto.

Scott mwenye umri wa miaka 30 aliamua kuanza kuitumia laptop yake akiwa ameiweka kwenye meza na matunda yake yalijionyesha baada ya miezi mitatu ambapo mkewe Laura ambaye naye ana umri wa miaka 30 alipopata ujauzito.

Hivi sasa ikiwa ni miezi 10 baada ya kuzaliwa kwa mtoto wao wa kike Taryn, Scott na mkewe ambao wanaishi kwenye mji wa Clanfield, Hants, bado hawaamini jibu la tatizo lao kuwa lilikuwa ni laptop.

"Sikuwahi kusikia kuhusiana na laptop kuharibu mbegu za kiume, nilishtuka sana", alisema Laura.

"Scott alikuwa akiitumia laptop yake kila siku jioni kwa masaa kadhaa akiwa ameiweka mapajani huku tukiangalia TV, hatukuwahi kufikiria kuwa ilikuwa na madhara na ilikuwa ikiharibu mbegu zake za kiume", aliongeza Laura.

Naye daktari bingwa wa masuala ya uzazi Sue Kenworthy alithibitisha madhara ya laptop kwa kusema kuwa wanaume inabidi watumie laptop wakiwa wameiweka kwenye meza badala ya kuiweka mapajani.
Previous
Next Post »