Wataalamu wa afya kote duniani wametoa wito wa kupiga jeki
juhudi za kukabiliana na chanzo kikubwa zaidi cha mateso na kutojiweza ambacho
ni magonjwa ya kiakili.
Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kutoa uhamasisho wa afya ya magonjwa ya kiakili duniani,wataalamu wa afya wanasema magonjwa ya akili ni moja wapo ya maradhi yanayopuuzwa sana, hasa katika nchi zinazokuwa.
Asilimia sabini na tano ya watu wanaokumbwa na magonjwa ya akili wanaishi katika nchi hizo zinazokuwa na wengi wao hawapati matibabu na huduma zinazofaa.
Takriban watu milinoni mia nne na nusu, wanakabiliwa na magonjwa ya akili huku thuluthi moja ya watu hawa wakiwa wanaishi katika nchi zinazostawi.
Kulingana na shirika la afya duniani, (WHO), watu wanane kati ya kumi wanaoishi katika nchi zonazokuwa, hawapokei matibabu hata kidogo.
Nchini Ghana wagonjwa wa kiakili, walio katika baadhi ya vituo vya matibabu, hunyimwa chakula na kuachwa uchi.
Nchini Afghanistan, familia nyingi zimemmpoteza mtu mmoja au zaidi katika kipindi cha miaka thelathini ambacho nchi hiyo imekabiliwa na vita.
Na inakisiwa kuwa takriban nusu ya wale walio na zaidi ya umri wa miaka kumi na tano, wana matatizo ya kiakili kama vile shinikizo la mawazo.
Nje ya mji mkuu wa Kabul hakuna hospitali hata moja ya kutoa matibabu kwa wagonjwa wa akili.
Hata hivyo Afghanistan haiko peke yake, kwani takriban nusu ya idadi ya watu duniani, wanaishi katika nchi ambayo ina mtaalamu mmoja wa matibabu ya kiakili anayewahudumia angalau wagonjwa 200,000.
Wameelezea changamoto ya ufadhili au misaada kwa taasisi za kuwahudumia wagonjwa hao hususan katika nchi maskini ambako magonjwa ya kiakili ni tatizo ambalo limepuuzwa
EmoticonEmoticon