Watuhumiwa wavurugu hizo wakipandishwa kwenye gari la polisi.
Picha na Mtaa kwa Mtaa Blog
Baadhi
ya vizuizi vilivyowekwa na waislam eneo la Mbagala Kizuiani wakati wa
maandamano yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo kupinga kitabu
kitakatifu cha Koran kufanyiwa dhihaka na mtoto Emmanuel Josephat ambaye
aliitemea mate.
Polisi wakiwa katika kuhakikisha hali ya usalama inaimarishwa katika eneo la Mbagala jana
Mmoja wa waandamanaji akiwa amekamatwana askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU)
Baadhi ya magari yaliyoharibika katika maandamano ya waislam
HAMISI
SALUM BABA MZAZI WA KIJANA AMBAYE MSAAFU WAKE ULIFANYIWA DHIHAKA NA
EMMANUEL JOSEPHAT NA KUZUA MAANDAMANO MAKUBWA YALIYOFANYWA NA WAAISLAMU
JIJINI DAR LEO.
Picha na Happy Mnale
DAR ES SALAAM, Tanzania
VURUGU
kubwa zimezuka baada ya mtoto Emanuel Josephat(14)’ kukojolea kitabu
cha Quraan cha dini ya kiislam limeingia katika hatua nyingine baada ya
waamini wa dini ya kiisilam kukusanyika wakishinikiza kuachiwa kwa mtoto
huyo ili wamuue.
Waamini
hao wanaokadiriwa kufikia idadi ya 3000 baada ya kutawanywa na Polisi
waliingia mitaani na kuchoma kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania(KKKT), Mbagala Zakhem, Kuharibu Kanisa la Anglican,kuvunja vioo
katika kanisa la Wasabato, huku kanisa la Tanzania Assembly of
God(TAG), Mbagala Kizuiani wakilichoma moto na kuchukua vifaa vya muziki
na kuviunguza hadharani.
Vurugu
hizo zilizotokea jana jijini Dar es Salaam, majira ya saa 5 asubuhi
ambapo waislamu hao walivamia kituo cha polisi Maturubai,Mbagala
Kizuiani.
Vurugu
hizo ambazo zimesababisha gari za polisi namba T142 AVV,PT 0966 na T
325 BQP,basi la uda na gari la waandishi wa habari kutoka Clouds
zikiharibiwa kwa mawe na waandamanaji hao.
Awali
waamini hao walikusanyika katika kituo hicho cha polisi wakimtaka mtoto
huyo ambaye alikuwa chini ya ulinzi aachiwe na Polisi walipogoma
kufanya hivyo ndipo vurugu hizo zilipoanza.
Kikosi
cha kutuliza ghasia kilionekana kuzidiwa nguvu na watu hao ambao
walikuwa wakiwatawanya kutoka eneo moja wanakimbilia eneo lingine na
kuleta madhara mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufunga barabara.
Hatahivyo
baada ya viongozi wa dini hiyo kufika wakiwa wameambatana na Sheikh wa
Wilaya ya Temeke, Sheikh wa Taasisi na Jumuiya za Waislamu kukaa kikao
na kamanda wa Polisi Wilaya ya Temeke, David Misime, walifikia muafaka
wa kuwaita waislamu hao na kuwatuliza lakini hali iliendelea kuwa si
shwari kwani baada ya viongozi hao kuona waandamanaji hao wakikamatwa na
kupigwa walikuja juu na kutishia kuondoka.
|
EmoticonEmoticon