Rais wa Venezuela Hugo Chavez ameshinda muhula wa nne
mamlakani baada ya mgombea wa upinzani Henrique Capriles kukubali
kushindwa katika uchaguzi uliofanyika siku ya Jumapili
Bwana Chavez alishinda uchaguzi huo kwa asilimia 54
Wafuasi wa Chevez walipiga mayowe, vifijo na nderemo katika mji mkuu Caracas, kusherehekea ushindi wake
Bwana Chavez, alisema ataendelea kuhakikisha
kuwa nchi hiyo imevuna matunda ya ujamaa na pia akaahidi kuwa
atajikakamua kuwa rais mzuri.
Rais wa tume ya uchgauzi Tibisay Lucena
alitangaza kuwa asilimia 90 ya kura zilizohesabiwa bwana Chavez
alishinda asilimia 54.42 huku mpinzani wake akichukua asilimia 44.97.
''Utawala wa mapinduzi umeshinda" bwana Chavez aliwaambia wafuasi wake waliokuwa wanamshangilia sana katika ikulu ya Rais.
"Viva Venezuela! Viva the fatherland! Alisema bwana Chavez. Kinyang'anyiro kilikuwa kikali na ushindi uko sawa.
Hata hivyo, Chavez pia alisikika akitoa kauli ya
kusema kuwa serikali yake itawajumuisha kila mwenye maono sawa na yeye.
''Ninajitolea kuwa rais bora kuliko nilivyokuwa katika siku za nyuma''
aliahidi Rais Chavez.
Mgombea mwenzake, bwana Capriles alimsifu na kumpongeza Chavez, na kuwaambia wafuasi wake wasihisi kama wameshindwa.
"nataka kumpongeza mgombea mwenzangu, rais wa nchi yetu'' alisema akiwa katika makao makuu ya kampeni yake.
Aliongeza kuwa "tumepanda mbegu nyingi,kote nchini Venezuela na ninajua mbegu hizi zitazaa miti mingi''
Wafuasi wa Chavez waliojaa furaha, walisherehekea katika barabara za mji mkuu wakipeperusha bendera.
Kwa upande wake, Henrique Capriles, alikubali kushindwa na kuwataka wafuasi wake kutovunjika moyo
Watu nchini humo wamepokea ushindi wa Chavez kwa
hisia mbali mbali. Edgar Gonzalez ambaye ni mfanyakazi wa ujenzi,
alisema '' siamini , nina furaha nyingi sana ''
Rais Chavez ni mmoja wa wakosoaji wakubwa wa
Marekani kutoka Amerika ya Kusini. Mshindani wake alimtaka afahamu kuwa
nusu ya watu nchini humo wanaotofautiana na sera zake. Bwana Chavez
aliugua maradhi ya saratani na kutibiwa nchini Venezuela ingawa sasa
hana tena maradhi hayo.
EmoticonEmoticon