WALIMU WATAKIWA KUACHANA NA MAMBO YA KISIASA.

Walimu wa shule za msingi na sekondari Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya wametakiwa kuachana na masuala ya kisiasa badala yake wajikite kwenye ufundishaji ili waweze kuinua kiwango cha elimu katika wilaya hiyo ambacho kimekuwa kikishuka mara kwa mara .

Imeelezwa kuwa baadhi ya walimu wamekuwa wakijihusisha na siasa kuliko kufundisha watoto na hivyo kupelekea kiwango cha elimu kushuka kwa wilaya ya Mbarali  na kwamba masuala ya siasa waachiwe wenyewe.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Mila Wilaya ya Mbarali Bw.mwanasimtwa mwagongo wakati alipozunguza na gazeti hili mwishoni mwa wiki kuhusiana na hali  ya elimu wilaya ya mbarali .

Bw. Mwagongo alisema baadhi ya walimu wamekuwa wakijihusisha na siasa wakati wao wapo ikwa ajili ya kutoa elimu kwa watoto  na si siasa kama ambavyo wengine wamekuwa wakifanya na kusahau kazi waliyopewa ya kutumikia taifa.

Alisema kuwa hakuna sababu  kwa walimu kuanza kupewa motisha wa kufundisha vizuri wakati kiwango cdha elimu hakiridhishi machoni kwa jamii na kuonekana wilaya ya Mbarali kuwa nyuma kielimu mara kwa mara.

“Hapa mimi binafsi sioni kama kuna umuhimu wa kutoa motisha kwa lipi sasa wakati kiwango cha elimu si kizuri kabisa na kinatia aibu ,watoto wetu wamebaki kufqanya vibarua tu badala ya kujali elimu kweli ndo tutoe zawadi mimi kwa  hili sikubaliani na hili”alisema.

Alisema kuwa kinachotakiwa kwa walimu ni kuacha kushabikia mambo yasiyowahusu hususani masuala ya siasa ambayo yana wenyewe wao wajikite katika kutoa elimu bora kwa watoto lakini si siasa ambayo mwisho wake si mzuri hasa kwa suala la elimu kwa ujumla.

Akizungumzia kuhusu wakuu wa idara ammbao wanakaa maofisini kusubiri taarifa za maendeleo ya wanafunzi katika shule mbali mbali alisema waache tabia hiyo  na badala yake watembelee katika shule  kujua kero za wanafunzi na walimu ili elimu iweze kupanda.

Wakuzungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa majina yao baadhi ya wananchi ya wilaya ya Mbarali walisema kuwa ili wanafunzi na walimu waweze kufanya vizuri ni vema wakaguzi wa shule wawe wanapita mara kwa mara  na kuachana na mfumo wa zamani wa kukagua wanafunzi pekee.

“Ikiwa ina maana ya kutambua changamoto zinazowakabili walimu katika ufundishaji  pamoja na utekelezaji wa majukumu yao”Walisema.
Previous
Next Post »