MTOTO KAZALIWA NA KITU KAMA MKIA NCHINI CHINA

 

Maajabu ya uumbaji yamemfanya mama mzazi wa Xiao Wei ambaye ni mchina amwage machozi akiomba msaada wa kunusuru maisha ya mwanae mwenye umri wa miezi 7 aliyezaliwa na  kitu kama mkia
Kitu hicho mathalani  kama mkia mfupi, wenye urefu wa sentimita 8 ( 8 cm ), katikati ya makalio mengine mawili.
Akiongea kwa uchungu, mama mzazi wa mtoto huyo amedai kuwa kwa muda mrefu amekuwa akiwaomba madaktari wafanye upasuaji wa  mkia  huo  lakini wao wamekuwa wakimjibu kuwa hiyo si kazi nyepesi kama anavyodhani
"Tukilikata litaota tena, hivyo hatutakiwi kukurupuka na badala yake tutakiwa kupata muda wa kupitia vitu vingi ukiwemo mrija wa uti wa mgongo ambapo  mkia huo umejitenganisha na makalio yake" .Alisema daktari mmoja akimjibu mama huyo
Previous
Next Post »