WATOTO WALAZIMIKA KUTEMBEA UMBALI MREFU KUFUATA ELIMU - MBEYA.

Watoto wa Kijiji cha Ilomba,Kata ya Masoko katika halmashauri ya Wilaya ya Mbeya wanalazimika kutembea umbali wa zaidi kilomita nane kwenda shule kutokana na kijiji hicho kutokuwa na shule hali inayopelekea hali ya elimu kwa kijiji hicho kuwa duni kutokana na umbali uliopo .

Kutokana na hali hiyo wananchi wa kijiji hicho wanalazimika kuwapeleka watoto wao kuandikishwa darasa la kwanza katika wilaya jirani ya Ileje.

Akizungumza na mwandishi wetu mmoja wa wajumbe wa serikali ya kijiji cha Ilembo Tarafa  ya Isangati Christopha Nkuwa amesema kuwa kijiji hicho ambacho kipo katika kata mpya ya masoko hakina shule na hakuna harakati zinazoendelea kijijini hapo.

Amesema kwamba kata ya masoko ambacho kipo kijiji cha Ilomba kimekuwa na matatizo mengi  ukiachana na kukosekana kwa shule pia kata hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa zahanati na
barabara inayounganisha vijiji vingine vya kata hiyo.

Kwa upande wake Diwani wa kata Ilembo Edward Mwampamba kijiji amesema kijiji hicho kina matatizo mengi kubwa zaidi ni kukosekana kwa zahanati ambayo ingewasaida wanakijiji hawa kupata tiba ndogo ngodo katika zahanati hiyo.

Hata hivyo wananchi wa eneo hilo wamekuwa wakitembea umbali wa kilomita 15 kwa miguu kwenda kufuata hudumu ya afya,wengine hufia njiani na akina mama wajawazito kujifungulia  njiani hali inayohatarisha usalama wa watoto.
Previous
Next Post »