Watu
wengi tunapenda matunda Fulani kwa ladha yake tuu bila kutaka kupata
faida, katika mwili ikiwa faida ya baadhi ya matunda ni pamoja na radha
yamatunda mabalimbali.
1. Tango ni chanzo kizuri cha vitamin B.
2. Tango huupa mwili na vitamin. Asilimia 95 ya tango ni maji hivyo huupa mwili maji na kuusaidia kuondoa sumu mwilini kwani pia lina vitamin karibu zote ambazo mwili huhitaji kila siku.
2. Tango huupa mwili na vitamin. Asilimia 95 ya tango ni maji hivyo huupa mwili maji na kuusaidia kuondoa sumu mwilini kwani pia lina vitamin karibu zote ambazo mwili huhitaji kila siku.
3. Tango pia hutumika kwenye matunzo ya ngozi/urembo ambapo huwekwa
machoni na kuondoa vimbe hasa kwa watu ambao umri umeanza kusogea kwani
tango lina virutubisho vya kuondoa vimbe hizi na pia lina silicon na
sulfur ambazo husaidia ukuwaji wa nywele.
4. Tango lina virutubisho kama lariciresinol, pinoresinol na secoisalariciresinol ambavyo kulingana na tafiti mbali mbali za magonjwa ya kansa husaidia kupunguza aina mbali mbali za kansa kama kansa ya matiti, kansa ya mifuko ya mayai kwa wanawake, kansa ya kizazi kwa wanawake na kansa ya tezi dume kwa wanaume.
5. Tango husaidia kuondoa harufu mbaya kinywani.
6. Tango huondoa hangover kwa watumiaji wa pombe kwani lina vitamin B
ambazo husaidia kupunguza ukali wa maumivu ya kichwa pale unapoamka
asubuhi ila unatakiwa kula kabla ya kulala ili uamke ukiwa vizuri.
7. Tango husaidia kupungua uzito na mmeng’enyo uende vizuri. Kutokana
na kiasi kidogo cha sukari kilichopo kwenye tango na kiasi kikubwa cha
maji, tango ni tunda sahihi kukusaidia upungue uzito. Kiasi cha maji
kilichopo kwenye tango na Kamba Kamba zake huusaidia mwili kuondoa sumu
katika mfumo wa chakula na kusaidia mmeng’enyo wa chakula. Unapokula
tango kila siku pia hukusaidia wewe mwenye choo kigumu au usiyepata choo
kabisa kwa muda mrefu kuondokana na tatizo hilo.
8. Tango husaidia wagonjwa wa kisukari, hupunguza mafuta mafuta
kwenye mishipa ya damu na huweza kudhibiti shinikizo la damu aina zote
mbili (Low and high blood pressure). Tango lina hormone ambayo
huhitajika kwenye chembechembe za kongosho (pancreatic cells) ilikuweza
kutengeneza insulin ambayo husaidia kudhibiti kiwango cha sukari kwenye
mwili hivyo kuwasaidia wagonjwa wa kisukari. Pia watafiti wamegundua
kuwa kuna kirutubisho kiitwacho sterol kwenye tango ambacho husaidia
kupunguza mafuta kwenye mishipa ya damu. Tango lina kiwango
kikubwa
cha potassium, magnesium na Kamba Kamba ambazo husaidia sana kudhibiti
shinikizo la damu aina zote yani high blood pressure na low blood
pressure.
Husaidia afya ya viungo, huondoa gout na ugonjwa wa baridi yabisi
(Arthritis). Tango ni chanzo kizuri cha silica ambayo inafahamika
kusaidia afya ya viungo kwa kuimarisha viunganishi vya viungo
(connective tissue). Pia tango lina Vitamin A, B1, B6, C & D,
Folate, Calcium, Magnesium na potassium ambavyo hufanya tango
linapochanganywa na juice ya karoti huweza kutibu gout na baridi ya
yabisi (arthritis) kwa kupunguza kiwango cha tindikali kwenye mkoo (Uric
acid).
10. Kutokana na maji na virutubisho vilivyopo kwenye tango, tunda hili husaidia kupunguza homa pale inapopanda.
Nadhani tutakuwa tumeelimika kwa kufahamu umhimu wa tunda aina ya tango
ikiwa tunda hili halivutii kula kwa kuwa halina radha nzuri sana pia
halina harufu inayosikia kuwa hili ni Tango kwa kukazia tango lina
asilimia kubwa ya maji.
Zingatia Madini ya Potassium yanayopatikana katika matango ndicho
chakula cha moyo kwa sababu huwezesha moyo kupiga mapigo katika hali ya
kawaida. Ulaji wa matunda na vyakula vyenye kiwango kikubwa cha
potassium kama tango ni muhimu sana hasa kwa mtu mwenye tatizo la moyo,
shinikizo la chini la damu.
EmoticonEmoticon