MAHUSIANO BORA NI MUHIMU KATIKA MAFANIKIO. |
Mtu
anaweza kuwa na uwezo mkubwa sana ndani yake na nguvu za kufanikiwa lakini
asifanikiwe. Naona unashangaa, ndiyo sijakosea unaweza ukawa na uwezo mkubwa wa
kufanikiwa lakini usifanikiwe kwa sababu ya kukosa mawasiliano mazuri na
wengine
Usiwe
na mawazo potofu haujalogwa, wala sio kwamba huna bahati. Lakini swali ni
kwamba je, unaishije na watu wanaokuzunguka?Je, unasaidianaje na wale watu
unaotaka wakusaidie kufanikiwa? Je, unawazungumziaje watu hao?
Ili
kufanikiwa ni lazima kujitengenezea mahusiano bora na wanaokuzunguka. Hata kama
ikatokea kuna wakati kutokuelewana, jaribu kujenga mahusiano yawe bora zaidi
hata kama unaona huna kosa kwako.
Mafanikio
mara nyingi sana yanajengwa na mahusiano bora Inapotokea pale mmekoseana kwa
namna fulani hivi, ni vyema kuvumiliana na kutambua kuweza kuishi na kila mmoja
kwa kujua mwenzangu anataka nini na kitu gani ambacho hakipendi ili mweze
kwenda pamoja katika safari ya mafanikio.
Siku
zote mahusiano bora ndiyo yatakayokuletea furaha na mafanikio ambayo unayataka
kila siku. Hakuna mtu anayeweza kukuharibia mafanikio yako zaidi wewe ufanye
hivyo kwa kuzidi kuharibu mahusiano yako na ya wengine. Mafanikio yoyote
hayajengwi na mtu mmoja. Bali yanajengwa kwa ushirikiano unaotakiwa kuuonyesha
kila siku.
Jifunze
na furahi kuwa sehemu ya mabadiliko kwa maisha ya watu wengine. Utafanikiwa kwa
hili ikiwa utajijengea mahusiano bora na wengine. Jiulize, je, unataka kuishi maisha ya
mafanikio na kutokata tamaa, basi njia rahisi jijengee mazoea ya kuwa na
mahusiano bora ya kudumu kila wakati.
Mawasiliano
na mahusiano ni nguzo pekee ambayo Mungu alikupa kupata mafanikio kwa urahisi.
Kumbuka unaweza kuamua kuwa wa tofauti kwa kuanza wewe kudumisha mahusiano bora
na wengine. Hiyo itakusaidia sana kujenga maisha yako na kuwa bora siku zote.
Nikutakie
siku njema na endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila wakati.
Makala hii imeandikwa na Noel Ngowi,
E-mail;
ngowi123@gmail.com
EmoticonEmoticon