Trump alaumiwa na wagombea wenzake kwa ghasia katika kampeni

Mgombea urais wa Republican,  Donald Trump akizungumza kwenye mkutano wa kampeni huko Boca Raton, Florida, March 13, 2016.
Wagombea urais wa Marekani wanajiandaa kwa ajili ya Jumanne wakati ambapo majimbo yenye wajumbe muhimu yanatarajiwa kufanya uchaguzi wao wa awali huku wote waliobakia kwenye kinyang’anyiro hicho wanamlaumu mgombea anayeongoza katika chama cha Republican, Donald Trump kwa ghasia ambazo zimezuka kwenye mikutano yake ya kampeni.
Uchaguzi wa awali katika majimbo ya Florida, Ohio, Illinois, Missouri na North Carolina ni muhimu kwa wapinzani wa Trump ambao wanataka kumzuia asisonge mbele kupata uteuzi wa chama kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwezi Novemba.
Lakini Trump alikanusha kwamba kampeni yake ilichochea ghasia akiuambia mkusanyiko huko Bloomington, Illinois siku ya Jumapili kwamba anataka amani na sio matatizo.
Previous
Next Post »