Kuandika
mpango biashara ni jambo muhimu sana ambalo unapaswa kulifanya ili
uweze kufanikisha biashara/kampuni yako kwa weledi wa hali ya juu. Aidha
mpango mzuri wa biashara husaidia kwa kiwango kikubwa uwezekano wa
kupata Mkopo na mtaji wa kuendesha biashara au kampuni kwa ujumla.
Zifuatazo ni hatua muhimu zakufuata katika kuandaa MPANGO BIASHARA
(BUSINESS PLAN)
Andika muhtasari katika ukurasa mmoja: huandikwa mishoni
kabisa maana ni ufupisho wa ulichokieleza lakini hua ndio ukurasa wa
kwanza kuonekena katika mpangilio.
Maono (vision)
Misheni (mission)
Dhamira (objectives)
Maelezo ya biashara au kampuni yako kwa kuweka, historia, usajili, waanzilishi, wamiliki,leseni
Elezea bidhaa au huduma utakazo zitoa ukieleza
Jinsi ya kutengeneza
Usindikaji
Bei
usambazaji jinsi ya kuitumia n.k
Elezea taarifa za masoko na hali ya ushindani wa bidhaa, uwezo
na mapungufu yaliyoko, na utofauti wa bidhaa yako na zilizopo tayari
Fafanua mkakati wa biashara yako
Wafanyakazi
Mgawanyo wa kazi
Muda wa kazi
Mashine
Vifaa
Jinsi ya kumfikia mteja
Makisio yako juu ya
mtaji unaouhitaji
mauzo kwa muda
faida na hasara zinazowezekana kutokea
mzunguko wa pesa
mcahanganuo wa kurudisha gharama na kupata faida
ulinganifu wa sehemu tofauti tofauti za biashara
viambatanisho ulivyonavyo kama leseni, cheti cha kulipa kodi,
risiti za mashine ulizonazo, mitambo, taarifa nyinginezo zilizo muhimu
ambazo hazijatajwa katika orodha hii.
EmoticonEmoticon