MKUU
wa wilaya ya Wang'ing'ombe Asumpta Mshama amesema kuwa tatizo la ufaulu
wa mtihani wa kidato cha nne mwaka 2015 kushuka linatokana na uzembe wa
walimu na sio wazazi wala wanafunzi linatokana na uzembe walimu
kujihusisha kimapenzi na wanafunzi pamoja na tabia ya baadhi yao
kujihusisha na mambo ya kisiasa.
Akizungumza katika kikao kazi kilichowakutanisha walimu wakuu wa shule za sekondari wilayani humo pamoja na wakuu wa bodi amesema kuwa shule nyingi wilayani humo zina mazingira mazuri ya kufaulisha yenye madarasa mazuri mabweni na maabara jambo ambalo amesema linaonesha kuwa wazazi wamehamasika kuchangia elimu lakini walimu ndiyo kikwazo.
Mkuu huyo wa wilaya ametumia kikao hicho kuwaagiza wakuu wa shule kuhakikisha wanawasimamia walimu kufundisha na kujiepusha na vitendo visivyofaa hasa mapenzi shuleni huku akiwaagiza kushirikiana na watendaji kuwafikisha kwenye vyombo vya kisheria wazazi ambao hawajawapeleka wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza.
Miongoni mwa sababu za ufaulu kushuka katika shule za sekondari wilayani humo imetajwa kuwa ni pamoja na walimu na wanafunzi kukosa chakula cha mchana, Muingiliano wa elimu na siasa huku wengine wakisema walimu wanajihusisha na shuguli za ujasiriamali na kilimo kama bodaboda.
Wakitoa taarifa za wanafunzi waliotakiwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2016 baadhi ya walimu wakuu akiwemo Optatus Mng'ong'o mkuu wa shule ya sekondari ya Wanging'ombe wamesema baadhi ya wanafunzi wametoroka pamoja na wazazi wao huku wengine wakiwa ni yatima pamoja na kueleza changamoto za mapokeo ya wazazi juu ya dhana ya elimu bure inaathiri maendeleo ya elimu.
Hata hivyo mkurugenzi wa wilaya hiyo Merkzedeki Humbe amesema walimu walio wengi wanapenda kukumbilia kujiendeleza kimasomo na kuacha shule zikiwa na mapengo ya walimu na hivyo ameagiza walimu wakuu kuhakikisha wanaruhusu walimu kwa kuzingatia uhitaji wa shule huku akieleza kuwa sifa ya mwalimu kupata nafasi ya kujiendeleza iwe ni kufaulisha kwa kiasi kikubwa..
Wilaya wanging'ombe ina shule za sekondari 17 na ufaulu wa mwaka 2014 ulikuwa ni asilimia 77 huku ufaulu wa mwaka 2015 ukishuka na kufikia asilimia 72 na idadi kubwa ya wanafunzi wamefeli kwa kupata madaraja ya 0 na 4.

EmoticonEmoticon