ZIJUE FAIDA ZA TIKITIMAJI MWILINI.




TIKITImaji ni miongoni mwa matunda yanayopatikana kwa wingi nchini ni tunda lenye virutubisho vingi vyenye faida kubwa katika mwili wa binadamu japokuwa asilimia 92 ya tikitimaji huwa ni maji.

Hata hivyo, asilimia 8 zilizobaki zina faida kubwa mwilini jambo linaloonekana kutofahamika kwa wengi. Tutaeleza baadhi ya faida chache kati ya tikitimaji.
Ndani ya tunda hili kuna Vitamin A, inayosaidia kuboresha afya ya macho na pia kuondosha sumu mwilini; Vitamin C, inasaidia kuboresha kinga, kuponya majeraha, kukinga uharibifu wa seli, kuboresha afya ya meno na fizi; na vitamini B6, inayosaidia ubongo kufanya kazi na pia kuibadilisha Protini kuwa nishati.
Tunda la tikitimaji lina kiwango kikubwa cha Lycopene kuliko tunda lolote au mboga za majani.

Ndani ya tunda hili kuna madini ya Potasium. Lina uwezo mkubwa wa kusaidia misuli na mfumo wa fahamu kwa ujumla kufanya kazi zake vizuri.
Tikitimama pia lina Amino Asidi na virutubisho vingine vinavyosaidia kurahisisha mtiririko wa damu kwenye mishipa yake.
Sifa ya kipekee iliyopo katika tunda hili ni ule uwezo wake wa kusaidia kupunguza ama kuondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Kwa kunywa juisi yake iliyokamuliwa bila kumenywa kwa maganda yake, kutaisadia kabisa kuondoa tatizo hilo.
Tunda hili limeonesha kulainisha vizuri mishipa ya damu na kufanya mzunguko wa damu mwilini kuwa mwepesi bila athari yoyote mbaya.
Kwenye tikitimaji kuna faida tangu kwenye majani, ganda na tunda na hata nyama yake.

Potassium iliyomo kwenye tikitimaji, huimarisha misuli ya mwili na huwafaa sana wanamichezo. Ulaji wa kipande kimoja baada ya kufanya mazoezi, huondoa tatizo la kukaza kwa misuli ya miguu, pia husaidia kupunguza uzito mwilini.
Tikitimaji lina kiwango kidogo sana cha kalori lakini lina kiwango kikubwa cha maji, hivyo kwa mtu anayetaka kupunguza uzito wa mwili linaweza kumsaidia kwa kula kwa wingi ambapo atakuwa anajisikia tumbo kujaa lakini bila kuwa ameshiba sana, hivyo kuwa rahisi kwake kujizuia na kula vyakula vingine hata kwa kutwa nzima na bila kuathirika kiafya.
Kirutubisho cha ‘Arginine’ kilichomo kwenye tikitimaji huchochea kwa kiasi kikubwa uimarishaji wa kinga ya mwili. Huondoa sumu mwilini, vilevile hufanya kazi muhimu ya uponyaji vidonda na kuondoa ‘Ammonia’ na sumu nyingine mwilini ambazo zinapozidi humfanya mtu kusikia uchovu na kusababisha ugonjwa wa ini na figo.
Tikitimaji pia hufaa kuliwa na wagonjwa wa presha kwani hushusha shinikizo la juu la damu, huongeza nuru ya macho, hutoa kinga kubwa dhidi ya magonjwa nyemelezi yakiwemo yale hatari kama vile kansa ya matiti, kibofu cha mkojo, mapafu na kansa ya tumbo
Previous
Next Post »