KWA NINI WATU WENGINE WANABAKI MASKINI?



Sababu zifuatazo zinaweza kuwa na ukweli mtupu;

1. Kushindwa kuamua haraka fursa zinapojitokeza kwao

2. Fursa kali Zikitokea wanaziona kama ni uongo na utapeli wa mjini

3. Kung'ang'ania kuajiriwa hata kama ajira hiyo hailipi

4. Kudhania unajua sana hivyo huoni jipya la kujifunza

5. Kukosa ujasiri wa kuanza. Unapanga mwezi huu au mwaka huu ntafanya hili au lile. Lakini mwaka unaisha hujaanza!!!

6. Kutokuwa na ndoto ya kiasi cha pesa unazotaka kwa siku, kwa wiki mwezi au mwaka. Unataka shs ngapi kwa siku? Wiki? Mwezi? Mwaka? Kwa nini unataka kiasi hicho? Matumizi yako ya lazima ni yapi? Ya starehe zako ni yapi?

7. Kununua vitu vya bei kubwa sana na visivyo na tija yoyote katika kuongeza kipato chako.

8. Kuwaza kwamba maendeleo yanapatikana uzeeni na siyo ujanani? Eti kumiliki mamilioni ya pesa mpaka uwe mzee kama Reginald Mengi vile.

9. Kufikiri eti huwezi kufanikiwa kuwa na fedha kuubwa mpaka uwe freemason au fisadi. Ujinga.

10. Kuwa na wategemezi kibao nyumbani kwako wakati kipato chenyewe kinatosha kula watu 2 tu kwa mwezi. Hatari!!

11. Kusubiri siku utakayopata pesa nyingi sana eti ndipo utafanya biashara hii au ile! Utasubiri sana.

12. Kutokuweka akiba yoyote kwa malengo ya maendeleo ya watoto na wajukuu zao.

13. Kufikiria kuwa kuna siku utapata msaada kutoka kwa wafadhili, serikali au wazungu au washikaji zako. Utangoja sana.

14. Kubadilisha mshahara wako au kipato chako kuwa mali ya ukoo mzima. Kila mtu kwenye ukoo wenu anakuomba pesa na wewe unampatia. Usimpe mtu samaki mfundishe kuvua samaki naye hatakuomba tena samaki. Usimpatie maziwa ndugu yako mfundishe kufuga ng'ombe wa maziwa.

Mpendwa wewe umeguswa na sababu ipi ktk hizo?

Nakutakia Februari Njema?
Previous
Next Post »