Mume wa zamani wa mwanamuziki maarufu Marekani Mariah Carey, rapper na mchekeshaji Nick Cannon ameamua kutoa ya moyoni baada ya mkewe kuvishwa pete ya uchumba na mwanaume mwingine bilionea James Packer.
Cannon na Mariah Carey ambao
walifanikiwa kupata watoto wawili mapacha waliachana mwaka 2015 baada ya
kutofautiana na kila mmoja kuendelea na mambo yake.
Mariah Carey aliingia kwenye uhusiano
mwingine na bilionea James Packer raia wa Australia na sasa wameingia
kwenye hatua nyingine ya uhusiano wao baada ya kuvalishana pete ya
uchumba.
Nick Cannon hakuonyesha kuumizwa na
uamuzi wa Mariah Carey na kuandika ujumbe ambao aliwapongeza wote kwa
uamuzi waliofikia na kuwatakia muunganiko mwema katika maisha yao mapya
EmoticonEmoticon