Mkali wa muziki na filamu nchini Marekani, Will Smith, amesema bado
ana ndoto za kuja kuwa rais wa nchi hiyo kwa miaka ijayo. Msanii huyo
ambaye anafanya vizuri katika filamu, ameamua kurudi tena kwenye muziki
baada ya kukaa kimya kwa miaka mingi, lakini mbali na kufanya muziki
amesema kuwa lengo lake ni kuja kuwa rais wa Marekani. “Ninaamini kila
kitu kinawezekana, lakini kwa upande wangu ni kwamba siku moja nije kuwa
rais wa Marekani, hii ni mipango yangu kwa kuwa ninaamini ninaweza
kuiongoza nchi. “Wazo la kuja kuwa rais lilikuja baada ya kufanya
mazungumzo na Donald Trump, ambaye amenishawishi kwa asilimia kubwa kwa
kuniambia kwamba hakuna kisichowezekana duniani kama una nia nacho, hiyo
ni kauli ambayo inanitia moyo kwa kiasi kikubwa,” alisema Smith.
EmoticonEmoticon