Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (RAHCO) Mhandisi Benhadard Tito (kulia).
Rais wa
Jamhuri ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hodhi ya rasilimali za
reli Tanzania (RAHCO) Mhandisi Benhadard Tito ili kupisha uchunguzi wa
kina kufuatia ukiukwaji mkubwa wa taratibu za manunuzi uliobainika
katika mchakato wa utoaji wa zabuni ya ujenzi wa reli ya kati.
Akitoa
taarifa kwa vyombo vya habari, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue
amesema, Rais Magufuli amefikia uamuzi huo baada ya kuitisha kikao cha
wataalamu kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za serikali ambazo
zinahusika katika utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Reli ya kati kwa
kiwango cha kisasa yaani “Standard Gauge”
Amesema
pamoja na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO, Rais Magufuli
ameivunja bodi ya RAHCO baada ya kujiridhisha kuwa haikutekeleza
ipasavyo wajibu wake katika kusimamia mchakato wa zabuni hiyo na badala
yake imeonekana kutetea kilichofanyika
Aidha
Rais Magufuli amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO Mhandisi Benhadard Tito
kutoa ushirikiano kwa vyombo vya serikali vitakavyofanya uchunguzi zaidi
kuhusu mchakato wa Zabuni hiyo.
Pia
ameiagiza Mamlaka ya udhibiti wa manunuzi ya umma (PPRA) kuchunguza na
kuchukua hatua dhidi ya kampuni za ukandarasi zilizopewa zabuni ya
ujenzi huo endapo itathibitika kuwa zimeshiriki katika ukiukwaji wa
sheria.
Katika
hatua nyingine Balozi Sefue amesema, Rais Magufuli amevunja bodi ya
Mamlaka ya Reli Tanzania (TRL) kutokana na kutoridhishwa na jinsi bodi
hiyo ilivyoshughulikia ripoti ya uchunguzi wa mchakato wa ununuzi wa
mabehewa ya treni.Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
22 Desemba, 2015.
EmoticonEmoticon