Nicky Minaj awatumbuiza raia wa Angola
Mwanamuziki
wa kufoka wa kizazi kipya kutoka Marekani Nicki Minaj aliwatumbuiza
maelfu ya mashabiki katika mji mkuu wa Angola Luanda licha ya shinikizo
kutoka kwa wanaharakati wa kupigania haki za kibinadamu asiandae tamasha
hilo la kusherehekea msimu huu wa Krismasi.
Wanaharakati
wa The Human Rights Foundation (HRF) walimuandikia barua totoshoo huyo
kutoka Marekani wakidai pesa alizolipwa zilitokana na 'faida ya upunjaji
wa mali ya umma na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu wanyonge nchini
Angola''.
Minaj mwenye umri wa miaka 33 alipuzilia mbali kampeini hiyo na kuandaa shoo ya kukata na shoka Jumamosi usiku.
Shoo hiyo
ya kufana iliandaliwa kwa hisani ya kampuni ya simu ya Unitel, ambayo
ni mali ya familia ya rais Jose Eduardo dos Santos.
Tangu
kukamilika kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe 2002, taifa hilo
linalozalisha mafuta mengi zaidi barani Afrika limeshuhudia ukuaji
mkubwa wa uchumi kutokana na utajiri wake mkubwa wa madini na mafuta.
Wanaharakati
wa The Human Rights Foundation (HRF) wanamtuhumu rais dos Santos kwa
kuwahujumu wenyeji kwa kujilimbikizia utajiri yeye na familia yake.
Aidha HRF
inasema kuwa Unitel ambayo inamilikiwa kwa kiwango kikubwa na mwanawe
rais huyo Isabel dos Santos inatokana na utajiri huo mkubwa usio halali.
Shoo hiyo ya kufana iliandaliwa kwa hisani ya kampuni ya simu ya Unitel
Isabel
dos Santos anayedaiwa kuwa ndiye mwanamke tajiri zaidi barani Afrika
aliorodheshwa majuzi katika jedwali la 15 watu wanaoendeleza ufisadi
mkubwa zaidi duniani.
Kabla ya kushuka dimbani, Minaj alipiga picha akiwa amejifunika bendera ya ya Angola na nyengine akiwa Isabel dos Santos .
sikujua kuwa ndiye mwanamke wa nane tajiri zaidi duniani.'' aliandika Minaj.
" Lol. Yikes!!!!! GIRL POWER!!!!!.BBC
EmoticonEmoticon