Nyumba na Makazi Yaendelea Kubomolewa Mbezi Beach, Kinondoni Dar......Tazama Video Hii Ujionee Ghorofa Hili Linavyoporomoshwa


Kijiko cha Manispaa ya Kinondoni kikibomoa nyumba ya Deus Kisisiwe iliyopo Block J Mtaa wa Libermann Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Ofisa wa Polisi akichukua picha wakati kijiko cha Manispaa kikiendelea na ubomoaji.
Manispaa ya wilaya ya Kinondoni kushirikiana na Wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi wakiwa wameweka tangazo lao katika ukuta wa uzio wakimaanisha eneo hilo lisitumike kwa maana ya maeneo ya wazi.
Nyumba nyingine eneo hilo nayo ikisubiri kubomolewa na manispaa ya Kinondoni.
Ubomoaji ukiendelea.
Familia ya nyumba inayotakiwa kubomolewa na manispaa wakitoa samani za ndani ili kupisha ubomoaji.
Ubomoaji ukiendelea katika maeneo ya Mbezi Bichi jijini Dar es Salaam.
Wazee wa kazi wakiwa katia geti la nyumba inayotakiwa kubomolewa maeneo ya mtaa wa Libermann Mbezi Bichi jijini Dar es Salaam
Ubomoaji wa uzio wa nyumba maeneo ya Libermann Mbezi Bichi jijini Dar es Salaam  mara baada ya kubisha hodi na kutokufunguliwa.
Uzio umebomolewa na watu wakiwa ndani kwaajili ya ubomoaji wa nyumba hiyo ambayo imejengwa maeneo ambayo ni ya wazi.
Magari yakiwa ndani ya nyumba inayotakiwa kubomolewa.
Magari yakitolewa nje ili kupisha ubomoaji wa nyumba maeneo ya Libermann Mbezi Bichi jijini Dar es Salaam .
Wenyeji wa nyumba ambayo imeanza kubomolewa uzio wakitoa vitu ndani ili kupisha ubomoaji wa nyumba hiyo.
Wakazi wa nyumba nyeupe inayobomolewa wakitoka nje ya nyumba baada ya kuanza kubomolewa na manispaa ya Kinondoni.
Wananchi wakihamisha vitu kupisha bomoabomoa.
Wananchi wanaangalia jinsi manispaa inavyobomoa nyumba Mbezi bichi jijini Dar es Salaam

Tazama  Video Ya Tukio

Previous
Next Post »