Jose Mourinho: Sina haki ya kusajili Januari


Jose Mourinho (kulia) amesema hana haki ya kusajili Januari
Jose Mourinho (kulia) amesema hana haki ya kusajili Januari
Kocha wa Cheslea Jose Mourinho amesema hana haki ya kusaini katika dirisha dogo la usajili mwezi Januari.
Mabingwa wa Ligi Kuu wamepoteza mechi saba kati ya 12 mpaka sasa wako nafasi ya 16 katika msimamo wa ligi.
“Nitakuwa mwenye furaha zaidi na kikosi hiki nilichonacho. Nina furaha na wachezaji wangu, nawaamini wachezaji,” alisema Mourinho.
Chelsea itawaalika Norwich siku ya Jumamosi, alisema:“Sisemi sitasaini kabis- ninasema sitaiomba klabu kufanya hivyo. Sina haki kufanya hilo, kwa maoni yangu.”
“Sitataka mabadiliko. Sitaiuliza bodi Januari,” aliongeza.
Previous
Next Post »