TEA YAIPA TET MKOPO WA SHILINGI BILIONI TATU KUANDAA MITAALA NA KUCHAPISHA VITABU VYA ELIMU YA MSINGI




Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Sifuni Mchome (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na Mamlaka ya Elimu (TEA) zilipotialiana saini mkataba wa makubaliano ambapo TEA itaipatia TET Mkopo wa Sh Bilioni 3 kwaajili ya kuandaa mitaala na kuchapisha vitabu vitakavyotumiwa na wanafunzi shule za msingi nchini kuanzia darasa la tatu hadi la sita. Prof Mchome, amewataka TET kuhakikisha wanakamilisha kazi hiyo kwa weledi ili kuweza kusaidia mabadiliko ambayo yatachangia kuwa na elimu inayokidhi viwango vya kimataifa.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa TEA, Joel Laurent na Kaimu Mkurugenzi wa TET, Dk Leonard Akwilapo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dk Leonard Akwilapo (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Joel Lauren (kulia) wakitiliana saini hati za makubalino ya mkopo wa Sh Bilioni 3 ambazo TEA itaipatioa TET. Katikati ni Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Sifuni Mchome.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dk Leonard Akwilapo (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Joel Lauren (kulia) wakionesha hati za makubalino ya mkopo wa Sh Bilioni 3 ambazo TEA itaipatioa TET baada ya kutiliana saini jana mbele ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Sifuni Mchome.Picha: Father Kidevu Blog.


Picha ya pamoja ya Wakurugenzi wa TEA, TET, Katibu Mkuu pamoja na watumishi wao.
 **************
Na Father Kidevu Blog
MAMLAKA ya Elimu Tanzania (TEA) imeipatia mkopo wa shilingi Bilioni 3 Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) katika makubaliano yaliyofikiwa leo Septemba 30, 2015 jijini Dar es Salaam.


Makubaliano hayo yalifikiwa mbele ya Katibu Mkuu Wizara ya Eklimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Sifuni Mchome ambapo TET itatumia fedha hizo katika kuandaa mitaala na kuchapisha vitabu vitakavyotumiwa na wanafunzi shule za msingi nchini kuanzia darasa la tatu hadi la sita.


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Joel Laurent amesema mkopo huo nafuu utakaolipwa katika kipindi cha miaka sita, umetolewa katika kutekeleza sera mpya ya elimu ya mwaka 2014.


“Mamlaka kwa kuzingatia Sera mpya ya Elimu ya mwaka 2014, imeridhia maombi ya mkopo ili kuhakikisha uwepo wa mitaala, muhtasari na vitabu vya kiada kwa darasa la tatu hadi la sita vinavyoendana na mahitaji na wakati,”alisema Laurent.


Utaratibu huo utaiwezesha TET kuandaa vitabu vya kiada kwa hatua ya kwanza ya elimu msingi, kutafanya uwepo wa mitaala inayoendana na kuwa kuboresha mfumo wa upatikanaji wa vitabu sahihi kulingana na mitaala nchi nzima kupitia TET hivyo Sasa nchi itakuwa na kuwa na kitabu kimoja cha kiada kwa shule nzima tofauti na ilivyo sasa kila shule zinavitabu vyake vya kufundishia.


Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dk Leonard Akwilapo alisema mkopo huo watautumia kufanya utafiti na kubaini mahitaji ya maboresho kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali wa elimu wakiwamo wanafunzi, walimu, wazazi na waajiri na kuandaa mitaala ya Elimu ya awali na Elimu ya Msingi kuanzia darasa la tatu hadi sita na kuandika vitabu vya kiada.


Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Sifuni Mchome aliwataka TET kuhakikisha wanakamilisha kazi hiyo kwa weledi ili kuweza kusaidia mabadiliko ambayo yatachangia kuwa na elimu inayokidhi viwango vya kimataifa.
Previous
Next Post »