NDEGE ya
mafunzo ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), imepata ajali
ikiwa na marubani wawili katika eneo la Silversands, Visiwa vya Bundya,
katika Mwambao wa Bahari ya Hindi Kaskazini Mashariki mwa Jiji la Dar
es Salaam.Taarifa
iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano, Makao Makuu ya
Jeshi, Upanga, ilisema marubani hao wanaendelea kutafutwa baada ya
kuzama habarini.
Tukio
hilo limetokea Oktoba mosi, mwaka huu, saa tatu 3:30 asubuhi ambapo
marubani waliopotea ni Luteni Kanali Talkisiyo Ndongoro na Kapteni
Gaudence Hamis.
Chanzo
cha ajali hiyo ni hitilafu ya injini ambapo baada ya marubani kugundua
hitilafu hiyo, walifanya juhudi za kujiokoa kwa kutoka katika ndege,
kuangukia baharini na kuzama.
EmoticonEmoticon