SIKU YA MWANAMKE WA ILEJE YAZINDULIWA RASMI MKOANI MBEYA



Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Jannet Mbene akizungumza na Wanawake waliohudhuria sherehe za siku ya Mwanamke wa Ileje  (Hawapo Pichani )katika ukumbi wa Mikutano CCM  Wilayani humo.Picha Jamiimojablog Mbeya 


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene( katikati)  na Mkuu wa Wilaya ya Ileje Rosemary Senyamule kulia wakifurahi jambo katika sherehe hizo .

Sherehe zikiendelea







Na Jamiimojablog.
Naibu Waziri wa Viwanda an Biashara Janeth Mbene  amezindua siku ya mwanamke wa Ileje ambayo imeanza kuazimishwa Oktoba mosi kwa kuwakutanisha wanawake kutoka katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kubadilishana uzoefu.

Pia maadhimisho hayo yanalenga  kujifunza masuala mbalimbali yakiwemo ya Afya, na  Uchumi ili kujikomboa kutoka kuwa tegemezi an kujitegemea kwa kipato.

Katika ufunguzi wake Mbene amewataka Wanawake wilayani humo kutuitumia vyema siku hiyo kwa kuha kikisha wana jadili changamoto zinazowakabili ili waweze kujikwamua kiuchumi kutoka walipo na kuwa katika hali nzuri kimaisha.

Mbene amewataka wanawake ambao ni nguzo ya familia kuziangalia changamoto walizonazo, ambazo alisema kila changamoto iliyopo wahesabu kama inawaathiri mara mbili (ni dozi mara mbili) hivyo lazima wao wenyewe wawe tayari kuzikataa kwa kushirikiana an wengine.

Amesema zipo fursa nyingi katika wilayani humo ambazo kama zinatumia vizuri zitaweza kuwanufa akina mama hao hivyo ni wakati wao kuzitumia fursa hizo ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Mbene ambaye pia ni mgombea ubunge kwa tiketi cha Chama cha mapinduzi (CCM)katika jimbo la Ileje amesema moja ya fursa ambayo  kama itatumia vizuri ianweza kuwainua akina mama hao ni pamoja na kuanzisha vikundi mbalimbali vitakavyo jihusisha na shughuli za kilimo cha mbogamboga.

Amesema kwamba ili wanawake waweze kujikomboa hawana budi kuanzisha miradi mbalimbali ya uzalishaji ili waweze kuondokana na hali ya kuwa tegemezi katika familia.

Hata hivyo amesema katika mikakati yake aliyojiwekea juu ya kuwakomboa wanawake hao atahakikisha anaangalia njia mbadala ya kuwakwamua kulingana na mazao wanayozalisha ili kuweza kukuza uchumi wao na kutunza familia ikiwa ni pamoja na kuanzisha miradi endelevu.

Mwisho


Previous
Next Post »