JAMII YAASWA KUTOKUTEGEMEA MISAADA KUTOKA NJE


Mwenyekiti wa Rotary Marathon na mtoa maada, Sharmilla Bhatt  katika mkutano (THURDAY TALK) unaofanyika kila Alhamisi ya kila mwezi unaoandaliwa na kampuni ya Solution Blocks jijini Dar es Salaam jana.

JAMII ya watanzania wanatakiwa kutokutegemea misaada kutoka nje ya nchi  isipo kuwa tunatakiwa kujitolea  ili kusaidia jamii isiyojiweza  kwa jia ya harambee.
Hayo yamesemwa na  Mwenyekiti wa Rotary Marathon na mtoa maada, Sharmilla Bhatt katika mkutano unaofanyika kila Alhamisi ya kila mwezi unaoandaliwa na kampuni ya Solution Blocks jijini Dar es Salaam jana.
alisema kuwa jamii  na makampuni binafsi yatambue kua katika jamii huu hii tunayoiishi kuwa kuna watu ambao hawajiwezi katika mahitaji yao ya kila siku na hivyo makampuni yanaweza kuandaa harambee kutok vyanzo vya ndani kwaajili ya kuisaidia jamii inayo hitaji bila kutegemea misaada kutoka nje ya nchi.

aidha alisema kuwa Oktoba 14 ambapo ni siku ya kumbukumbumbu ya Mwalimu Julius Kamabarae  Nyerere  kutakua na matembezi ambayo yatakua na uchangiaji wa jamii.
Baadhi ya wadau waliohudhulia mkutano (THURDAY TALK) uliondaliwa na kampuni ya Solution Blocks wakimsikiliza mtoa maada katika hoteli ya Colesium jijini Dar es Salaam jana.
 Baadhi ya wadau wakiwa katika mkutano (THURDAY TALK) uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.
 Mshiriki wa mkutano (THURDAY TALK) uliofanyika jijini Dar es Salaam jana akiuliza swali kwa mtoa maada. 
Mwanzilishi wa kampuni ya Solution Blocks, Msomisi Mbenna akiwakaribisha baadhi ya wadau mbalimbali katika mkutano (THURDAY TALK) wa kila Alhamisi ya kila mwezi uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. 
 Wadau wakisikiliza kwa makini maada iliyokua ikijadiliwa.
  Meneja wa masoko wa Hoteli ya Colloseum akiwakaribisha wadau katika mkutano (THURDAY TALK)ulioandaliwa na kampuni ya Solution Blocks jana jijini Dar es Salaam.

 
Previous
Next Post »