Mgombea
wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dkt. John Pombe
Magufuli akihutubia umati wa watu kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika
katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo, akiendelea na kampeni zake
za kuisaka Ikulu nchini Kote huku akiwaomba Watanzania kumpigia kura za
ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi wa Rais, Wabunge na
Madiwani ili aweze kuwatumikia kwa uaminifu mkubwa.PICHA NA MICHUZI
JR-DODOMA
Akitoa
hotuba yake katika moja ya mikutano yake alioufanya katika mji wa
Kibaigwa Dk. John Pombe Magufuli amesema hakuna kitu kinachomuumiza kama
mauaji ya wakulima na wafugaji yanayotokea kati ya wilaya za Kongwa
Mkoani Dodoma na Kiteto mkoani Manyara.
Dkt
Magufuli ameahidi kuwa mara baada ya kuchaguliwa na kuunda Serikali
yake,jambo hilo atalipa uzito wa juu na kulifanyia kazi kwa umakini
mkubwa. “Yaani Mimi Magufuli Nimteuwe Waziri na watendaji wengine wa
serikali halafu Mauaji yatokee watu wafe, Mkuu wa mkoa yupo , Mkuu wa
wilaya yupo na Kamanda wa Polisi yupo wabaki wanapunga upepo, wamiliki
wa Ng’ombe wabaki wanakula maisha haiwezekani,nitalala nao mbele
na Ng’ombe wataliwa msibani kwa uzembe waliousababisha”,alisema
Magufuli kwa msisitizo mkubwa.
Magufuli
amewataka wafugaji na wakulima kuishi kwa amani bila kubaguana, lakini
pia akasema atatumia sheria za ardhi na kuhakikisha maeneo ya wafugaji
na wakulima yanatengwa, ili wafanye shughuli zao na kukuza kipato na
uchumi wao bila kusumbuliwa.
Baadhi
ya wananchi wa mji wa Dodoma na vitongoji vyake wakimsiiliza Dkt
Magufuli alipokuwa akinadi sera zake za kuomba kura ili kushika nafasi ya Urais ya awamu ya tano.
Waziri
Mkuu wa zamani, Jaji Mstaafu Joseph Warioba, akimnadi Dkt.Magufuli kwa
kuhubiri amani katika mikitano yake ya kampeni kuliko wagombea wa vyama
vingine hawasisitizi kudumisha amani nchini jambo ambalo ni tunu ya
taiafa
Dkt.
Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa Dodoma Mjini,mara baada ya
kumkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM, Ndugu Anthony Mavunde wakati wa
mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Jamhuri mjni Dodoma leo.
Dk Magufuli akimnadi Mgombea ubunge Jimbo la Mpwapwa, George Lubeleje,mjini MPwapwa katika uwanja wa mgambo.
Mgombea
urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akimnadi Mgombea ubunge
Jimbo la Kongwa, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai wakati wa mkutano wa
kampeni jimboni humo.
Mawaziri wakuu wa zamani, John Samuel Malecela na Jaji Mstaafu Joseph
Sinde Warioba wakifuatilia mkutano wa kampeni wa Dkt Magufuli alipokuwa
akiwahutubia wananchi wa Dodoma kwenye mkutano wa kampeni.
Mgombea
urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli, akimsimamia Mgombea
ubunge Jimbo la Mtera kupitia CCM, Livingstone Lusinde aliyekuwa
akifanya mazoezi ya Push Up wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja
wa Jamhuri, Dodoma.
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa akimuombea kura Dk Magufuli wakati
wa mkutano huo wa kampeni mjini Dodoma jioni ya leo.
Walemavu nao wana haki ya kuwasikiliza Wagombea nafasi mbalimbali ikiwemo ya Urais,Ubunge na Udiwani
Wananchi
wa Kibaigwa wilayani Kongwa, wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM,Dkt.
Magufuli alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa kampeni mjini Kongwa.
Mgombea
Urais Dkt John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri Mkuu wa
zamani Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba,mjini Kibaigwa wilayani Kongwa
kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Wananchi wa Kibaigwa wilayani Kongwa wakifuatilia hotuba za Dkt Magufuli kwenye mkutano wa kampeni.
Dk Magufuli akijipigia kampeni kwa wakazi wa Kibaigwa , wilayani Kongwa .Akiwa
wilayani Kongwa, Dk Magufuli amesema kuwa akishinda urais atahakikisha
anadhibiti mapigano kati ya wakulima na wafugaji yanayoendelea nchini
na kusababisha vifo vya watu wengi
Dkt. Magufuli akiwapungia mikono wananchi alipowasili kwenye kampeni Uwanja wa Jamhuri Dodoma .
EmoticonEmoticon