Umewahi kumsikia huyu jamaa anaitwa ALIBABA kwa jina halisi Jack Ma japo Jack sio jina lake la kuzaliwa alipewa na marafiki anaitwa Ma Yun.
Huyu alishatajwa na forbes kuwa ni tajiri wa 18 duniani,mchina wa kwanza kuingia list ya matajiri duniani.Na mwaka 2014 akatajwa the richest man in china.Huyu bwana alitokea familia ya kawaida tu ya wanamuziki wa majukwani baba na mama.Akiwa mdogo alipenda kujifunza kiingereza akiendesha baiskeli yake kutoka kwao kwenda kujifunza English takriban miaka 8.
Alikuwa na hobby ya kutengeneza marafiki wa mtandaoni wale pan pals kama na wewe ulipitia hivyo kujikuta anatengeneza marafiki wengi ulaya na marekani.
Alijaribu kuingia chuo na kufeli mara 3 mfululizo ikabidi aingie chuo cha ualimu na hatimae akaja kuwa mwalimu wa literature akifundisha kiingereza.
Alibaba alipenda mambo ya Internet na akajikuta anatengeneza website kwa Msaada wa marafiki wanaoishi Marekani. Akajikuta anaanza kutengenezea makampuni website huko China.Na hii ilianza mwaka 95 alipotembelea marafiki zake Marekani ndio walimfundisha.
Website ya kwanza ilikuwa ni kuhusu China na ilimchukua masaa 5 kuitengeneza.Habari zake nikavuma na yeye kuona kuna fursa kwenye Internet business hivyo yeye na mkewe wakaanzisha Internet company na ndani ya miaka mitatu wakawa wameingiza dola 800,000
Mwaka 1999 Alibaba akaamua kujikita zaidi kwenye biashara hii ya Internet. Ofisi ikiwa ni apartment anayoishi akiwa na wenzake 17.
Alibaba ni nini?yaani huu ni udalali wa mtandaoni any bidhaa unayotaka nenda Alibaba. Com utaikuta. Ina hudumia zaidi ya viwanda ml 79 duniani na nchi zaidi ya 250
Kuna darasa lake moja niliona anafundisha vijana namna ya kutimiza ndoto zao.
Anasema hakikisha miaka ya 25 unautumia ujana vizuri kutimiza ndoto zako na jifunze kadri uwezavyo.Ukifikisha miaka 30 anza kuwaza kujiajiri mwenyewe ukiwa chini ya ajira.Ukifikisha miaka 40 jiajiri mwenyewe na fanya kazi na vijana.Ukifikisha miaka 50 mpaka 60 acha vijana wakufanyie kazi wakati kampuni yako imekuwa na umetoa ajira kwa vijana.
Umepata Somo gani toka kwa Alibaba???
#maishaclass
EmoticonEmoticon