Mkurugenzi
Mkuu wa Takukuru nchini, Dkt. Edward Hoseah akizungumza katika sherehe za
uzinduzi wa jengo la ofisi mpya ya TAKUKURU Mkoa wa Mbeya ambapo amesema kuwa Taasisi
hiyo imeweza kufanikiwa kupambana na rushwa kwa kiasi kikubwa
ambapo jumla kesi kubwa za rushwa 1,993 kuanzia mwaka 2004-2015 zimeweza
kufunguliwa ambazo ni sawa na ongezeko la asilimia 81 ikilinganishwa na kesi
384 zilizokuwepo miaka 10 ilioyopita (1995-2004) .
Amesema
,ongezeko
hilo la kesi kubwa limetokana na jitihada za Taasisi hiyo katika kupambana na
kuzuia rushwa nchini hasa katika kipindi cha serikali ya awamu ya nne, chini ya
rais Jakaya Kikwete.
|
EmoticonEmoticon