Mahakama nchini Misri imewahukumu waandishi watatu wa
kituo cha runinga cha Al jazeera miaka mitatu jela.
Wakati wa kutolewa kwa hukumu hiyo, Mohamed Fahmy, Peter
Greste na Baher Mohamed walipatikana na hatia ya kutangaza habari za uongo na
kulisaidia kundi la Muslim Brotherhood ambalo kwa sasa linatambuliwa kuwa kundi
la kigaidi.
Baher Mohamed pia alihukumiwa kifungo kingine cha miezi
sita.
Hata hivyo Peter Greste, yuko nje ya nchi baada ya kutimuliwa kutoka nchini humo mwezi Ferbruari.
EmoticonEmoticon