Utawala wa
kifalme nchini Swaziland unaongozwa na mfalme Mswati umetakiwa kufutilia
mbali sherehe maarufu za kitamaduni baada ya wasichana kadha waliokuwa
wakisafiri kwenda kwa sherehe hizo kufa kwenye ajali ya barabarani.
Kundi
linalounga mkono demokrasia nchini humo la (the Swaziland Solidarity
Network) limetoa wito kwa mfalme Mswati kufutilia mbali sherehe hizo
ambazo wasicha walio nusu uchi hucheza mbele ya mfalme. Image caption Wasichana wakicheza densi Kundi
hilo linasema kuwa zaidi ya wasichana 60 waliangamia wakati lori
walilokuwa wakisafiria lilihusika kwenye ajali ya barabarani. Utawala nchini Swaziland unasema kuwa idadi ya wasichana waliokufa ni 13.
EmoticonEmoticon