Staa wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ ameendelea kushusha maneno
kwa chama kinachounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) baada ya
kufunguka hadharani kuwa hawakuwa na sera ambazo zingemfanya aendelee
kubaki.
Staa huyo ambaye kwa sasa amerudi Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema kurudi kwake CCM hakumaanishi kama amehongwa kama watu wanavyoendelea kusambaza habari hizo bali amekwenda kutokana na kuvutiwa na sera.
“Naomba nieleweke kuwa dhamira yangu ya kubaki Ukawa ndiyo ilikuwa ikinisuta. Nikiwa kama mmoja wa wasanii, nimevutiwa na sera za CCM hasa kwa upande wa wasanii ambapo Mgombea Urais, Magufuli (John Pombe) alisema moja ya sera zao ni kujali maslahi kwa wasanii na kuwafungulia mfuko maalum utakaowashughulikia,” alisema Ray.

EmoticonEmoticon