Aunt Ezekiel: Nina Haki ya Kuhama Chama


MWIGIZAJI mahiri wa filamu nchini, Aunt Ezekiel, amedai kutishiwa amani baada ya kufanya maamuzi yake kisiasa ambapo amehamisha ushabiki wake kutoka chama kimoja na kwenda chama kingine.

Licha ya mrembo huyo kudai kupokea vitisho mbalimbali, pia alidai amehama chama hicho na kujiunga na kingine

kutokana na kukubali sera za chama hicho.

“Sera za chama nilichohamia zimenivutia na wala sikulazimishwa na mtu wala sijapokea fedha wala gari kuhamia

huko kama inavyosemekana, bali nafsi na mapenzi pamoja na haki yangu ndiyo yaliyonipeleka huko.

“Nashangaa maamuzi yawe yangu bado watu wanitumie jumbe za vitisho, mimi ni raia kama walivyo wengine,

umaarufu wangu usiwe sababu,” alisema Aunt, ambaye awali alikuwa akivaa magwanda yanayoaminika kuwa jezi ya chama alichokihama

Chanzo:Mtanzania
Previous
Next Post »