Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na aliyekuwa Mbunge
wa Ulanga Mashariki, Celine Kombani (56),amefariki dunia Jana nchini
India .
Kombani
alipitishwa na Chama cha Mapinduzi kutetea jimbo lake la Ulanga
Mashariki na alipita bila kupingwa katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba
25 mwaka huu.
Taarifa
kutoka ofisi za Bunge zimethibitisha kifo hicho na kueleza kwamba mwili
wa marehemu unategemewa kuwasili Dar es salaam siku ya Jumatatu, ambapo
Bunge na Serikali zitasimamia maandalizi yote ya maziko na kumsafirisha
kwa mazishi nyumbani kwa marehemu huko Mahenge ambako alikuwa Mbunge wa
jimbo la Ulanga.
R.I.P C. KOMBANI
EmoticonEmoticon