Baada ya utafiti huu kutoka chumba cha habari kilipitia page za Twitter za Wagombea Urais na vyama vyao kutazama kama kuna walichoandika baada ya kupata haya matokeo.
Mgombea Urais Edward Lowassa ambaye yuko kwenye tiketi ya CHADEMA ameyaandika haya kwenye page yake halali ya Twitter
‘Watanzania tusipumbazwe na tafiti ambazo hatujashiriki, tushiriki kwa mafuriko Oktoba 25, majibu ya kweli tutayapata‘
Dr. Magufuli hakuwa ameandika chochote kuhusu utafiti huu huku tweet yake ya mwisho ikiwa inaeleza furaha yake kwa jinsi Wananchi wa Bukoba walivyojitokeza kumsikiliza.
Wananchi wa Bukoba nimefarijika pasipo na wasiwasi kwa namna mlivyojitokeza kwa wingi kukiunga Chama Cha Mapinduzi.
Kwa upande wa ACT Wazalendo, kiongozi wake Zitto Kabwe aliandika kwenye Twitter ‘Chama chetu kinaamini kwenye tafiti haijalishi zina matokeo mazuri au mabaya kutuhusu, tumepokea matokeo haya kama changamoto… tutaongeza nguvu yetu kuhakikisha tunapata asilimia zaidi kwenye kura‘
Our party believe in research and accept results whether positive to us or not. Our trust in @Twaweza_NiSisi work is unshakable
January Makamba wa CCM kwenye sehemu ya Tweets zake aliandika kwamba hajashangazwa na matokeo ya utafiti wa TWAWEZA sababu imeendana na utafiti na CCM ambao ulitangazwa siku chache kabla.
I'm not surprised by Twaweza poll that gave @MagufuliJP a resounding 65% against Lowassa's 25%. It is consistent with our internal research.
EmoticonEmoticon