Mfuko wa
Bima ya Afya nchini (NHIF) umeingia makubaliano ya udhamini wa bima ya
afya kwa wachezaji na viongozi wa benchi la ufundi kwa vilabu 16 vya
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Akiongea
na waandishi wa habari katika mkutano uliofnayika leo ofisi za TFF
zilizopo Karume, Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine amesema
wanaishukuru NHIF kwa kuwapa udhamini huo ambao utavisaidia vilabu vya
Ligi Kuu katika matibabu ya wachezaji na bechi ka ufundi.
Tumekua
na kilio cha muda mrefu juu ya vilabu vya Ligi Kuu kuwa na Bima za afya
kwa wachezaji, kitu ambacho kipo kikanuni lakini vilabu vilikuwa
vinashindwa kutimiza hitaji hilo la kikanuni na sasa TFF kwa kushirikian
na NHIF tutakua tumeiondoa tatizo hilo.
Naye Mkuu
wa Mawasiliano wa NHIF, Sungi amesema udhamini huo wa bima ya matibabu
kwa wachezaji na benchi la ufundi utatolewa kwa matibabu yote
yatakayofnayika ndani ya nchi.
Mchezaji
au kiongozi pindi atakapopata tatizo la kuumwa, basi ataweza kutibiw
akatika hospitali yoyote yenye huduma ya Bima katika eneo alilopo, lengo
ni kuhakikisha wanakua na afya njema kwa ajili ya kushiriki vizuri
mikikimikiki ya Ligi Kuu ya Vodacom.
Lengo
letu ni kuona wachezaji wanapata huduma ya afya popote wanapokuwa na
kuweza kushiriki vizuri katika michuano ya Ligi Kuu, na kuweza
kuzitumikia vyema timu zao kwenye mashindano.
Ofisa
Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura kwa niaba ya vilabu vya Ligi
Kuu amesema wanashukuru kupata udhamini huo wa bima ya afya, uwepo wa
NHIF umevipunguzia vilabu mizigo wa matibabu na sasa vilabu vitaweza
kushiriki vizuri kwenye michuano ya msimu huu.
EmoticonEmoticon