Baadhi ya wakuliwa wa mkoani
Shinyanga, wakiwa na maofisa wa Agrics wakati wa mafunzo na uingiaji mkataba wa
makubaliano yliofanyika Kijiji cha Ishololo, Wilaya ya Shinyanga Vijijini. Warsha
hiyo iliongozwa na Lazaro Japhet (aliyesimama wa tatu kushoto mstari wa mbele.
Zaidi ya wakulima 12,000 wanataraji kufaidika na mbegu za mahindi na alizeti
kutoka Kampuni ya Agrics.
Mahindi yaliyooteshwa kisayansi na kampuni ya Agrics kwa
lengo la kuthibitisha ubora wa mbegu zinazotolewa kwa wakulima wa kanda ya
ziwa. Zaidi ya wakulima 12000 watanufaika na mbegu izo msimu huu. Matokeo ya
vipimo yalisadifu ubora wa kampuni ya Agrics kwa kutoa asilimia 100% ya ubora.
Kufuatia msimu mpya wa kilimo
unaotarajia kuanza hivi karibuni. Kampuni ya Agrics inatarajia kuwanufaisha
wakulima 12,000 wa Shinyanga vijijini, Maswa na Meatu kwa kuwapatia mbegu bora
za mahindi, alizeti pamoja na mbolea ili kuhakikisha kilimo biashara
kinainuliwa na kuleta tija kwa mkulima. Mbegu hizo zitatolewa hivi karibuni ili
kuhakikisha mkulima anakuwa na maandalizi ya uhakika msimu huu. Kampuni ya
Agrics hutoa mbegu kwa mkopo nafuu unaolenga kumnufaisha mkulima kwa mazao
mengi zaidi.
Pia Agrics ikishirikiana na
viongozi wa serikali huwanufaisha wakulima kwa kuwapatia mafunzo katika ngazi
tofauti za ukuaji wa mazao ili kuhakikisha mavuno yanasadifu malengo ya
wakulima hao.
Akiongea kwa niaba ya kampuni
ya Agrics, Meneja Miradi Bw. Charles Laswai alithibitisha ubora wa mradi huo
wakati akikabidhi mikataba ya uchaguzi wa mbegu kwa wakulima. ‘’ Ni miaka mitano
sasa tangu Agrics ianze kutoa mbegu bora kwa mkopo kwa wakulima wetu wa kanda
ya ziwa.
Kwa sasa wakulima wameelewa
zaidi umuhimu wa kilimo biashara. Mkulima anavuna zaidi ya asilimia arobaini
kulinganisha na kabla ya kujiunga na mradi huu wa kukopeshwa mbegu na mbolea
kwa ajili ya kilimo bora. Na kwa mwaka huu tunategemea mavuno mazuri zaidi
kwani hali ya hewa itakuwa nzuri kutokana na vyanzo vya taarifa ya hali ya hewa
nchini’’.
Wakulima wamekuwa wakikutana
na changamoto mbalimbali zikiwemo ukosefu wa mikopo kwa ajili ya kilimo na
ukosefu wa elimu juu ya kilimo bora chenye tija. Agrics ikiwa kama chachu ya
mabadiliko kwa mkulima wa kanda ya ziwa, imekuwa ikiwakopesha mbegu na mbolea zilizothibitishwa
kwa ubora, mkulima hutoa asilimia kumi wakati wa kuomba aina ya mbegu aitakayo
na badae hutoa asilimia 15 wakati wa kukabidhiwa mbegu husika.
Mkulima hupewa nafasi ya kuwa
huru na kusimamia kilimo chake huku akiendelea kupata mafunzo na ushauri kutoka
kwa afisa miradi wa Agrics ili kuhakikisha malengo ya mkulima yanatimia na
anazalisha kwa kiasi kikubwa. Mkulima humalizia asilimia 75% ya deni lake kwa
awamu tatu zinazompa muda wa kutosha baada ya kuwa amevuna.
“Ni kampuni ya Agrics
iliyoyabadilisha maisha yangu kufikia mafanikio haya niliyonayo. Kiujumla wamebadilisha
maisha ya wakulima wa hapa kijijini na kutufanya tuuage umasikini. Nilikuwa nikivuna
gunia nne katika hekari moja lakini kwa sasa navuna zaidi ya gunia kumi
kulingana na muitikio wa mvua. Tangu kujiunga na Agrics nimewapeleka watoto
watatu sekondari na ninamiliki pikipiki kutokana na mavuno yangu. Sijawahi
kuishiwa chakula kwani huwa ninaweka SIMIYU NA SHINYANGA.
akiba ya kutosha kwa ajili ya
familia yangu’’. Alieleza Bw. Steven Kanogu mkazi wa kijiji cha Ishinabulandi
wilaya ya Shinyanga vijijini wakati akipokea mkabataba wa mkopo wa mbegu na mbolea
kwa ajili ya kilimo cha msimu huu.
Agrics Ltd ni kampuni ya
kibiashara inayofanya kazi zake kwa kushirikiana na shirika la ICS. Agrics
inawapa wakulima wadogo wa kanda ya ziwa nchini Tanzania na Kenya fursa ya
kujipatia mbegu bora na za kisasa kwa mkopo nafuu unaolipwa kwa awamu zinazompa
mkulima nafasi nzuri ya kujiendeleza. Pia Agrics inahakikisha akiba ya chakula
kwa mkulima ni lazima kwa ajili ya kupunguza njaa kwa wakulima. Kwa mawasiliano
Zaidi tembelea tovuti yetu www.agrics.org.
EmoticonEmoticon