Watu zaidi ya 48 wameuwawa katika shambulizi, Al-Shabab wahusishwa


Watu zaidi ya 48 wameuwawa katika mashambulizi ya risasi yaliyonywa dhidi ya raia wa mji wa Mpeketoni karibu kabisa na kisiwa cha Lamu, Jumapili.
Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia BBC kuwa mashambulizi hayo yalifanyika kuanzia saa mbili usiku  wakati wakazi wa eneo hilo wakiangalia kombe la dunia na kudumu kwa masaa kadhaa na kwamba watu walishuhudia magari na nyumba vikiwaka moto.
Inaaminika kuwa wapiganaji hao zaidi ya 50 waliofanya mashambulizi walikuwa wapiganaji wa kundi la Al Shabaab japo kundi hilo halijatoa tamko lolote kuhusu uhusika wao.
Kenya imekuwa ikishambuliwa na kundi la kigaidi la Al Shabaab tangu mwaka 2011 walipoamua kupeleka wanajeshi wao Somalia kumbana na wanamgambo wa kundi hilo.
Previous
Next Post »