SHIRIKA
la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) limewatahadharisha
wananchi kuepuka taarifa za uzushi zilizoripotiwa na vyombo kadhaa vya
habari juu ya usambazaji maji machafu kwenye line za mabomba ya wateja
wa Dawasco.
Akizungumza
na gazeti hili, Kaimu Meneja Uhusiano wa Dawasco , Bi Everlasting Lyaro
alisema taarifa hizo za uzushi zimesambazwa na watu wachache ili
kuchafua taswira ya shirika hilo na pia kuihusisha Dawasco moja kwa moja
na mlipuko wa kipindupindu ulioingia jijini.
“Tunawatahadharisha
wateja wetu kuwa ubora wa maji unaozalisha na Dawasco unakidhi vigezo
vyote kwa matumizi ya binadamu na viumbe hai, hatuwezi kuzalisha maji
yenye kuleta madhala kwa wananchi kwani hata haki za binadamu haziruhusu
kufanya hivyo ” alisema Lyaro.
‘Ukweli
wa maeneo yanayolalamikiwa kama vile Ilala mitaa ya Sharif shamba na
Buguruni ni kuwa kuna kampuni za uchimbaji mifereji bado hatujabaini
kama ni ya watu binafsi au za manispaa.
Wao
walichimba mifereji ya majitaka karibia na mabomba ya wateja walio na
line za Dawasco za majisafi hivyo kutiririsha majitaka kwenye mfumo wa
majisafi. Ikapelekea maji machafu kuingia kwenye line zao na kupelekea
mabomba ya maji yanapofunguliwa zinakutana na yale maji machafu
yaliyokatwa kutoka kwenye mifereji” aliongezea lyaro.
Alisema
kuwa Baada ya kupokea malalamiko hayo tulichukua hatua kadhaa moja ni
kuchukua sampuli za Maji hayo na kwenda kuyapima na kurudi kufunga maji
hayo yasiendelee kutoka. Na baada ya upimaji sampuli ile na kukuta sio
salama tulitenga line(isolate) ya majisafi ya sharif shamba hadi hapo
tatizo litakapotatuliwa na mamlaka husika.
Tuhuma za
Dawasco kusambaza Maji machafu ziliripotiwa mapema wiki hii huku
zikihusishwa zaidi na athari za ugonjwa wa kipindupindu unaoendelea
kushika kasi jijini dar.
EmoticonEmoticon