TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA
WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 30.09.2015.
·
MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA KISHA
MWILI WAKE KUTELEKEZWA KANDO YA BARABARA.
·
WATU WANNE WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI
YA GARI KUGONGANA NA PIKIPIKI.
·
MTU MMOJA AFARIKI DUNIA NA WENGINE
KUJERUHIWA BAADA YA GARI WALIOKUWA WAKISAFIRIA KUACHA NJIA NA KUPINDUKA.
KATIKA
TUKIO LA KWANZA:
MTU
MMOJA MKAZI WA MAJENGO MAPYA JIJINI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MWANDAMBO SHUNYA (54) AUAWA KWA KUPIGWA
NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA NA KISHA MWILI WAKE KUTELEKEZWA KANDO YA BARABARA.
MWILI
WA MAREHEMU ULIKUTWA KANDO YA BARABARA MNAMO TAREHE 29.09.2015 MAJIRA YA SAA
23:30 USIKU HUKO ENEO LA MAJENGO MAPYA, KATA YA NSALAGA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI
NA MKOA WA MBEYA.
MWILI
WA MAREHEMU ULIKUTWA NA MAJERAHA KICHWANI NA USONI HUKU UKITOKWA DAMU NYINGI.
CHANZO NI KIPIGO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
UPELELEZI UNAENDELEA.
KATIKA
TUKIO LA PILI:
WATU
WANNE WAFARIKI DUNIA BAADA YA GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.519 AKH AINA YA TOYOTA HAICE IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA KUGONGANA
NA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.535
AWC AINA YA T-BETTER ENEO LA NANENANE JIJINI MBEYA.
AJALI
HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 29.09.2015
MAJIRA YA SAA 22:30 USIKU HUKO ENEO
LA NANE-NANE, KATA YA ISYESYE, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA
KUU YA MBEYA/NJOMBE.
WATU
WALIOFARIKI KATIKA AJALI HIYO NI 1.
MWENDESHA PIKIPIKI AMBAYE BADO KUFAHAMIKA JINA LAKE NA WATU WATATU RAIA WA
ETHIOPIA AMBAO MAJINA YAO BADO KUFAHAMIKA, JINSI YA KIUME AMBAO WALIKUWA
WAMEPAKIZWA KWA PAMOJA KWENYE PIKIPIKI HIYO KWA MTINDO MAARUFU WA MSHIKAKI.
AIDHA
KATIKA AJALI HIYO MTU MMOJA AITWAYE EDWARD
ALOYCE (42) MKAZI WA UYOLE ALIYEKUWA ABIRIA KWENYE HAICE ALIJERUHIWA NA
AMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA GARI NA
PIKIPIKI. DEREVA ALIKIMBIA BAADA YA TUKIO, JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA. MIILI
YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
KATIKA
TUKIO LA TATU:
MTU
MMOJA MKAZI WA MASOKO WILAYA YA RUNGWE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA TUKUPYELESYA ENOCK MWAKIFUNA (54)
AFARIKI DUNIA BAADA YA GARI WALIOKUWA WAKISAFIRIA YENYE NAMBA ZA USAJILI T.913 AMB AINA YA TOYOTA HILLUX
IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA KUACHA
NJIA NA KUPINDUKA.
AJALI
HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 29.09.2015
MAJIRA YA SAA 18:30 JIONI HUKO
KIJIJI CHA MASOKO, KATA YA MASOKO, TARAFA YA PAKATI, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA
MBEYA KATIKA BARABARA YA TUKUYU/LWANGWA.
AIDHA
KATIKA AJALI HIYO, ABIRIA WATATU WANAWAKE WAWILI NA MWAMAUME MMOJA WALIJERUHIWA
NA WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA RUNGWE. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO
KASI. DEREVA ALIKIMBIA NA KUTELEKEZA GARI BAADA YA TUKIO.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA
NA KUFUATA SHERIA/ALAMA NA MICHORO YA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
AIDHA
ANATOA WITO KWA WANANCHI/ABIRIA KUTOKUBALI KUPAKIZWA ZAIDI YA ABIRIA MMOJA @
MSHIKAKI KATIKA PIKIPIKI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA USALAMA
WAO. KAMANDA MSANGI ANATOA RAI KWA
ABIRIA KUTOA TAARIFA PINDI WANAPOONA DEREVA WA GARI/PIKIPIKI ANAENDESHA BILA
KUFUATA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI.
KAMANDA
MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE
TAARIFA ZA MAHALI ALIPO DEREVA WA GARI ALIYEKIMBIA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA
KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
Imesainiwa
na:
[AHMED
Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon