Hivi una habari kwamba usipojua kuchagua utajiri kila siku utachaguliwa na umaskini kila siku?
Vijana tunakula njaa ya nguvu miaka mingi kwasababu ya matatizo mawili.
1) hatujui kutambua fursa zikiwa mbele yetu kwasababu tuko bize kutafuta MTU wa kutusaidia badala ya MBINU ya kutusaidia.
2)
tukishapata fursa ya kutoka kimaisha, tunaichukulia poa badala ya
kuikumbatia kama vile ni pumzi yetu ya mwisho, na kuchukua hatua zote za
kuhakikisha haipotei kabla haijazaa matunda.
Wewe
ambae bado unasota kila siku kutafuta maisha, umejiuliza ni wapi
unakosea? Safari yako ina ramani yoyote au unaenda tu ilimradi uwe
unatembea?
Kwenye mkesha wa leo, chukua hatua ya kutafuta MBINU ya kukufikisha unapotaka kwenda.
Na
hatua hiyo ni kujibu kwanza swali lifuatalo: nikiwa nimefikia malengo
yangu, maisha yangu yatakuaje kuanzia niamke asubuhi hadi nilale jioni?
Simulia maisha hayo.
*************************************************************
Matarajio
yanayojengwa kwa wapiga kura Vijana ni makubwa MNO. Ukweli utabaki
hakuna Chama wala Serikali itakayoleta maendeleo mlangoni. Ni kwa
jitihada na kazi.
EmoticonEmoticon