Wanawake wa kijiji cha Endanachan katika kata ya Endamilay wilayani Mbulu mkoani Manyara wapata adha ya kukabiliana na wanyama wakali kama vile fisi nyakati za usiku kufuata matibabu.

Wanawake wa kijiji cha Endanachan katika kata ya Endamilay wilayani Mbulu mkoani Manyara wameilalamikia serikali na wanasiasa waliowahimiza kujenga zahanati katika kijiji hicho kwa lengo la kuepukana na vifo kwa akina mama wajawazito na watoto wakiwemo wazee wanaoshindwa kutembea umbali wa zaidi ya km 10 kufuata matibabu na badala yake ahadi hiyo imeshindwa kutelekezwa kwa miaka saba huku wakipata adha ya kukabiliana na wanyama wakali kama vile fisi nyakati za usiku kufuata matibabu.
Previous
Next Post »