![]() |
Moja kati ya matukio ya kujichukulia sheria mkononi yaliyowahi kutokea nchini. |
Kituo
cha sheria na haki za binadamu Tanzania LHRC leo wametoa Report ya Haki
za binadamu kwa kipindi cha nusu mwaka huu wa 2015 report ambayo
inaonyesha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu katika Nyanja
mbalimbali.
Taarifa
hiyo ambayo ni matokeo ya Tafiti mbalimbali zilizofanywa na kituo cha
sheria na haki za binadamu LHRC inaonyesha kuwa swala la haki ya kuishi
kwa watanzania bado imeendelea kukiukwa ambapo katika utafiti huo
unaonyesha kuwa kwa kipindi cha nusu mwaka pekee watu takribani 366
waliuawa kutokana na raia kujichukulia sheria mkononi jambo ambalo
limetajwa kuangamiza maisha ya watanzania walio wengi.
Mtafiti kutoka kituo hicho ndugu PAUL MIKONGOTI akizngumza na wanahabari wakati akitoa ufafanuzi wa Report hiyo leo Jijini Dar es salaam |
Akitoa
ufafanuzi juu ya Report hiyo mtafiti kutoka kituo hicho ndugu PAUL
MIKONGOTI amesema kuwa matatizo ya kujichukulia sheria mkononi yamekuwa
yakiwahusisha zaidi watu wanaokuwa na tuhuma za wizi,na hasa vibaka,huku
akisema kuwa matukio mengi ya kujichukulia sheria mikononi yamekuwa
hayatolewi taarifa kwenye vyombo vya habari hasa matukio yanayotokea
vijijini.
Mauaji
mengine ambayo yamejitokeza katika report hiyo ni mauaji ya askari hasa
wawapo kazini,ambapo kwa kipindi hiki cha nusu mwaka vituo vinne
vilivamiwa na kusababisha vifo vya askari watatu jambo ambalo
limeendelea kugarimu maisha ya askari hao.
Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za Binadamu LHRC Bi HELLEN KIJO BISIMBA akifafanua jambo |
Tofauti
na haki ya kuisha ambayo imejitokezaa katika Report hiyo iliyotolewa
leo haki nyingine ambazo zimeonekana kukiukwa kwa hali ya juu ni pamoja
na haki za wanawake na watoto,haki ya bkiupata habari na uhuru wa
habari,haki ya afya bora,haki ya kupiga kura,pamoja na maswala ya rushwa
na utawala bora yamejitokeza sana katika report hiyo.
Akizungumzia
Report hiyo mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu
LHRC Bi HELLEN KIJO BISIMBA amesema kuwa swala la kujichukulia sheria
mkononi limezidi kuwa kubwa na imefika kipindi sasa kwa watuhumiwa wa
kuchukua sheria mkononi na wale wa mauaji yatokanayo na imani za
kishirikina washughulikiwe kama wahalifu wengine kwa mujibu wa sheria za
nchi jambo ambalo linaweza nkupunguza hali hiyo
Aidha
ameishauri serikali kuhakikisha kuwa inarekebisha mfumo wa utoaji wa
haki unaboreshwa ili kutopa haki kwa wote huku ikiendelea kushirikiana
na wadau mbalimbali ili kurekebisha mkifumo hiyo.
Taarifa
iliyotolewa leo imejikita zaidi katika maeneo machache ya haki za
binadamu ambayo yameoinyesha kuwa na ukiukwaji wa hali ya juu katika
kipindi cha nusu mwaka ambapo taarifa kamili ya hali ya haki za binadamu
nchini itaandaliwa mwishoni mwa mwaka.
EmoticonEmoticon