Aliyekuwa
Mbunge wa Jimbo la Kahama mkoani Shinyanga, James David Lembeli,
akizungumza na waandishi wa habari Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Dar es
Salaam leo asubuhi wakati akitangaza kuondoka katika Chama Cha Mapinduzi
(CCM) na kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
Pamoja na kutangaza nia ya kugombea ubunge kupitia chama hicho.
Lembeli akizungumza na wanahabari.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
Wanahabari wakimsikiliza Lembeli. Suleiman Msuya
Na Mwandishi Wetu
ALIYEKUWA
Mbunge wa Kahama James Lembeli, amehamia rasmi Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Tukio
hilo la kuhama lilifanyika jijini Dar es Salaam Jana asubuhi katika
Hoteli ya Blue Pearl, Ubungo Plaza ambapo aliambatana na mwanae ambaye
alijitambulisha kwa jina Wizilya James.
Akizungumzia
uamuzi wake huo Lembeli alisema amekuwa ndani ya CCM kwa miaka yake
yote lakini kutokana na vitendo vinavyofanyika ndani ya chama hicho
ameaona akae pembeni.
Lembeli
alisema, ndani ya CCM ili ufanikiwe kupita michakato yote sahihi ni
lazima utoe rushwa au kuiba kura jambo ambalo yeye analipiga vita hivyo
kutofautiana na viongozi wa chama ngazi ya Wilaya.
"Ndani ya
CCM rushwa imekuwa ibada inasumu kali kuliko ukimwi hivyo nimeshindwa
kuvumilia naona Chadema wana viashiria vinavyofanana na mimi ngoja
tukafanye kazi," alisema Lembeli.
Alisema
katika harakati za kupata wagombea katika jimbo la Kahama kila mwaka ni
lazima rushwa itumike lakini chama kimekuwa kimya na kuwabeba wale watoa
rushwa.
Mbunge
huyo alisema ushahidi wa watu kutoa rushwa hasa katika kipindi hiki
umeonekana lakini wahusika wameendelea na hatua zingine bila kukemewa.
"Mimi
mwaka 2010 nilikuwa nimekatwa lakini huruma ya Rais Jakaya Kikwete
nilirejeshwa sasa nimeona hakuna sababu ya kuendelea kulazimisha kama
viongozi hawakutaki," alisema.
Alisema
iwapo angechukua fomu CCM mkakati ambao ulikuwepo ni kumkata kwa kile
ambacho wanaamini kuwa amekuwa akisimamia misimamo ambayo ina madhara
kwa Serikali.
Lembele
alisema kutokana na dhana hiyo ni vema aende katika chama ambacho
kinaonekana kuwa wabunge wake wanauchungu na nchi yao na sio kubebana
kusiko na sababu.
"Kufanya
kosa sio kosa lakini kurudia kosa ni kosa kubwa sana hivyo siwezi
kurudia kosa la 2010 hivyo huku Chadema ndiko sahihi," alisema.
Alisema ukiona mwenzako ananyolewa ni vema kujiandaa kwa kutia maji nywele jambo ambalo ameliona na ameamua kufanya hivyo.
"Siwezi
kutoa rushwa kwa sababu sijafunzwa hivyo na hata wananchi wa Kahama
wanajua kuwa mimi sio mtoa rushwa hivyo ukiwa hutoi rushwa CCM ni ngumu
kukubalika jambo ambalo linafanya kuwa rushwa iwe mbaya kuliko ukimwi,"
aliongezea.
Akizungumzia
kugombea ubunge kupitia Chadema, alisema atafanya hivyo kwani ukweli ni
kuwa anakubalika kwa wananchi wote kutokana na misingi yake ya
utumishi.
Alisema
mpaka anafanya uamuzi huo ameshafanya utafiti ambapo anaamini kuwa
atashinda tena kwa kishindo kwani wananchi wa jimbo hilo wanamkubali.
Lembeli
alisema kimsingi jimbo la Kahama wapinzani wapo tangu yeye akiwa Mbunge,
hivyo anaamini kuwa iwapo atafanikiwa kushinda hatapata wakati mgumu
kufanya kazi.
"CCM
imefanya mambo mengi ambayo kimsingi hayana afya ndani ya chama ukiwa wa
kwanza kwa kura ndani ya CCM unakuwa wa mwisho hali ambayo inakatisha
tamaa na hilo lilitokea 2010 na Chadema wakapata ushindi," alisema
Pia
alisema amepokea simu na meseji nyingi ambazo kutoka kwa wananchi
zinamtaka agombee kupitia chama Chadema hivyo pamoja na ukweli kuwa ni
uamuzi mgumu ila hawezi kula matapishi.
Alisema
ilimchukua masaa 10 kumuelezea mama yake juu ya uamuzi huo lakini baadae
alielewa hivyo kwa sasa ana baraka zote za mama na familia kwa ujumla.
Kuhusu uhusiano na 4U Movement
Akizungumzia
kuhusu uamuzi huo kuhusishwa na kundi la 4u Movement, alisema kimsingi
kundi hilo analiona kupitia mitandoa ya kijamii ila hana uhusiano nalo
na hahitaji kuwa katika hao.
Lembeli
alisema wananchi wa Kahama ni watu makini wanajua nini cha kufanya hivyo
uamuzi ambao watafanya utakuwa ni kwa uelewa wao na sio kwa msukumo wa
kundi hilo linalotajwa kuwa ni wafuasi wa Waziri Mkuu wa zamani Edward
Lowassa.
Kuhusu
Katiba iliyopendekezwa Lembeli alisema yeye ni muumini wa Serikali tatu
na alionesha hilo katika vikoa vyote vya bunge lile ambapo alikuwa
katika kamati namba moja.
Alisema
kutokana na ukweli huo ni dhahiri kuwa ameenda chama ambacho wanafanana
kifra kwani bila Serikali tatu hatma ya Tanzania itakuwa mashakani.
"Kwa hili
siwezi kubadilika mimi msimamo wangu hadi leo ni Serikali tatu ambapo
pia ni msimamo wa Chadema hivyo wengi ndio walishinda lakini mimi sio
mmojawapo," alisema.
Aidha
Lembeli alitumia muda huo kufafanua ni kwanini alitoa hoja ya kutaka
Lowassa na wengine ambao wamekutana na majanga ndani ya bunge wasafishwe
ambapo alisema haki haikutendeka kusafisha watu baadhi na wengine
kuachwa.
Lembeli
alisema katika taarifa ya Operasheni Tokomeza haikusema mawaziri fulani
wanamakosa ila iliweka bayana kuwa kulinga na nafasi zao wanapaswa
kuwajibika kisiasa.
Alisema mfumo wa kusafisha watu fulani na wengine kuwaacha sio mzuri kwani hauendani na misingi ya haki za binadamu ni ubaguzi.
Kwa upande wa mtoto wake wa pili Wizilya James Lembeli alisema wanamuunga mkono baba yao kwa uamuzi huo na kuwa wako nyuma yake.
Alisema
uamuzi ambao amechukua baba yake ni mgumu hasa ukilinganisha na kipindi
husika lakini hakuwa na njia nyingine kwani ni mtu wa siasa.
Akizungumzia
ujio huo Ofisa Habari wa Chadema ambaye ndiye alimpokea Lembeli alisema
kimsingi mwanachama huyo mpya alikiwa ni mpinzani kiroho hivyo hawana
shaka naye.
Makene
alisema wanaamini kuwa wamepata mtu ambaye anapenda mabadiliko kwani
alionekana ndani ya bunge na nje kwa kusimamia rasilimali za nchi bila
uoga.
Alisema
Chadema itaendelea kupokea wanachama wapya kutoa CCM na vyama vingine
hadi Julai 25 kwani lengo lao ni kuhakikisha kuwa nchi inafikia kwenye
mabadiliko chanya.
Lembeli
amekuwa Mbunge wa jimbo la Kahama, tangu mwaka 2005 hadi 2015 ambapo
awali alikuwa mwandishi na mtumishi katika shirika la Hifashi ya Taifa
(Tanapa).
EmoticonEmoticon