Mgambo wa Almashauri ya jiji la Mbeya wakiwa wameweka ulinzi mkali katika geti kuu la kuingilia wafanyakazi..(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Wafanyakazi wa Almashauri ya jiji la Mbeya wakiwa wamesimama nje wakisubiri nini kitaendelea..(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Mgambo wa almashauri wakielekea kufungua Mageti mara baada ya kukubaliana na Mkurugenzi wa Jiji.(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Wafanyakazi wakikimbia camera mara baaada ya kufunguliwa Geti.(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
ASKARI mgambo
wa halmashauri ya Jiji la Mbeya,leo wamefunga geti kuu la ofisi za halmashauri
ya Jiji na kuzuia wafanyakazi kushindwa kuingia ndani wakishinikiza kulipwa
mishahara yao ya miezi miwili pamoja na kutatuliwa kwa kero mbalimbali
zinazowakabili askari hao.
Askari hao
zaidi ya 20 wakiwa ndani ya ofisi za halmashauri hiyo, waligoma kufungua geti
kuu hilo kwa zaidi ya masaa mawili na kusababisha kero kwa watumishi na wateja
mbalimbali ambao waifika kupata huduma.
Akizungumza na
Mtanzania,mmoja wa kiongozi wa askari hao Athanas Samsoni, alisema wao wameamua
kufunga geti hilo na kuzuia watumishi kwa lengo la kuushinikiza uongozi ambao
ndio mwajiri wao kuwalipa mishahara yao pamoja na posho mbalimbali.
Alisema, mbali
na madai hayo pia mwajiri huyo amekuwa akishindwa kuwashonea sare za kazi jambo
linalosababisha kujitegemea hivyo kuendelea kuwaweka kwenye mazingira magumu ya
kiuchumi.
Alisema, wao
wanachokihitaji kutoka kwa mwajiri wao ni kulipwa mishahara yao pamoja na
kutekelezewa mahitaji yao muhimu kama vile sare na posho.
Akizungumzia
tatizo hilo, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Dk. Samweli Razalo alikiri kwa
halmashauri hiyo kutowalipa mishahara askari ho mgambo na kwamba suala lao
linashughulikiwa.
“Madai yao ni
ya msingi na wanaidai halmashauri mshahara wa miezi miwili Mei na Juni, uongozi
ulishakaa na viongozi wa askari na kuwaeleza lakini tunashangaa kuona leo
wamechukua uamuzi wa kufunga geti,”alisema.
Mwisho.
EmoticonEmoticon