Na Simon Chimbo
Watu
wengi walipata kuyaona maandishi yaliyopo mbele ya T-shirt ya ndani ya
mshambuliaji Carlos Tevez ambayo huonesha pale anaposhangilia goli,
Fuerte Apache.
Fuerte
Apache ni mtaa uliopo huko Buenos Aires Argentina. Hapa ni makao makuu
ya uhalifu. Sio sehemu nzuri kuishi, pombe, madawa na uporaji wote hapa
ndio ulipozaliwa, hapafai. Fuerte Apache ndio mtaa aliozaliwa
mshambuliaji mwenye nguvu Carlos Tevez. Ni sehemu wanaishi watu masikini
sana nchini Argentina.
“Ilikua
ni kipindi kigumu sana kuishi Fuerte Apache, usiku unapoingia, giza
kali, huwezi kutazama hata dirishani, ilikua inaogopesha sana. Huwezi
kutembea hata mtaani, ni hatari” anasema Carlos Tevez
Kitu
kilichobakia kumbukumbu kwake ni kovu lake la shingoni, uso na hadi
kifuani. Ilikua ni ajali akiwa na miezi kumi tu tangu azaliwe aliungua
na maji ya moto yaliyokua yakichemka jikoni.
Ilikua
ni ajali mbaya kwa Tevez ambaye aliugulia kwa kipindi cha miezi
miwili. Tevez hata alipoanza kucheza soka aliamua kutunza kovu lake
kama nembo ya uhalisia wa maisha yake na alikotoka.
Akicheza
katika klabu yake ya kwanza kabisa kama mchezaji wa kulipwa, Boca
Junior alikataa kulitoa kovu hilo. West Ham pia walijaribu kutaka
kumfanyia matibabu ili kumuweka sawa lakini amebaki na kumbukumbu hiyo.
Tevez alivunjwa meno katika ugomvi na wenzake mtaani kwao Fuerte Apache utotoni.
Tevez
anasema anashukuru amechagua njia sahihi kwani angeweza kuwa mharifu,
muuza unga na ukabaji lakini soka limemtoa na sasa sio masikini tena
anaishi kwa amani.
EmoticonEmoticon